Marko 4:1-12
Neno: Bibilia Takatifu
Mfano Wa Mbegu
4 Wakati mwingine tena Yesu alianza kufundisha kando ya ziwa. Watu wengi walikusanyika wakasongamana mpaka ukingoni mwa ziwa. Ikambidi Yesu aingie kwenye mashua, akaketi humo. 2 Akawafundisha mambo mengi kwa kutumia mifano na katika mafundisho yake akasema:
3 “Sikilizeni! Mkulima mmoja alikwenda kupanda mbegu zake. 4 Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani; ndege wakaja wakazila. 5 Nyingine zilianguka kwenye mwamba ambapo kuli kuwa na udongo haba; zikaota haraka. Kwa kuwa udongo haukuwa na kina, 6 jua kali lilipowaka zilinyauka na kukauka kwa kuwa hazi kuwa na mizizi. 7 Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga kwahiyo hazikuzaa matunda.
8 Na mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua; zikazaa matunda; moja thelathini, nyingine sitini na nyingine mia moja.” 9 Kisha Yesu akasema, “Mwenye nia ya kusikia na asikie.”
Kwa Nini Yesu Alitumia Mifano
10 Alipokuwa peke yake, baadhi ya wale waliokuwepo, pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili, walimwuliza kuhusu mifano yake. 11 Akawaambia, “Siri ya Ufalme wa Mungu imefunuliwa kwenu, lakini kwa wale walioko nje ya Ufalme wa Mungu, kila kitu husemwa kwa mifano 12 ili: ‘Kutazama watazame lakini wasione, kusikia wasikie lakini wasielewe. Kwa maana kama wangesikia na kuelewa wangegeuka na kutubu, wakasamehewa.’ ”
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica