55 Makuhani wakuu na wajumbe wote wa Baraza walijaribu kutafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo, lakini ushahidi wao haukupatana.

57 Ndipo watu fulani wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo wakisema, 58 “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitabomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga lin gine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59 Lakini hata hawa, ushahidi wao ulipingana.

60 Kuhani Mkuu akasimama mbele ya Baraza akamwuliza Yesu, “Huwezi kujibu mashtaka haya ambayo watu hawa wameleta juu yako?” 61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?” 62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu ya mbinguni.”

63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.

Read full chapter