Yesu Anatabiri Kubomolewa Kwa Hekalu

13 Alipokuwa akitoka nje ya Hekalu, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, ona jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo maridadi!”

Yesu akamjibu, “Unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, yote yatabomo lewa.”

Yesu Anawaambia Wafuasi Wake Wajiandae Kwa Mateso

Alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni akiliangalia Hekalu, Petro, Yakobo na Yohana walimwuliza faraghani, “Tafadhali tuambie, mambo haya yatatokea lini, na ni ishara gani zitaonyesha kuwa karibu yatatimia?” Yesu akaanza kuwaeleza: “Jihadharini mtu asije akawadanganya. Wengi wata kuja wakilitumia jina langu na kusema, ‘Mimi ndiye’ na wata wadanganya wengi. Na mkisikia habari za vita na uvumi juu ya vita, msishtuke. Mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho utakuwa bado. Mataifa yatapigana na falme kushambuliana. Matetemeko ya ardhi yatatokea sehemu mbalimbali na kutakuwa na njaa. Lakini huu utakuwa kama maumivu ya mwanzo tu ya uchungu wa uzazi. Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watu watawapeleka mahakamani na mtapigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ndipo mtaweza kutoa ushuhuda kuhusu Habari Njema. 10 Lakini kabla mwisho kufika, Habari Njema itahubiriwa kwa mataifa yote. 11 “Mtakapokamatwa na kupelekwa mahakamani, msihangaike kuhusu mtakalosema. Semeni lo lote litakalowajia wakati huo, kwa sababu maneno mtakayosema si yenu bali yatatoka kwa Roho Mtaka tifu.

12 “Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 13 Kila mtu atawachukia kwa ajili yangu; lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.

Read full chapter