Habari zil imfikia Herode mtawala wa Galilaya kuhusu miujiza iliyokuwa iki fanyika, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka!” Wengine wakasema, “Ni Eliya ametutokea” na wengine kwamba, “Mmoja wa manabii wa kale amefufuka.” Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa, ni nani huyu anayefanya maajabu haya ninayoambiwa?” Akajaribu sana amwone Yesu.

Read full chapter