Luka 9:57-62
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Kumfuata Yesu
(Mt 8:19-22)
57 Walipokuwa wakisafiri pamoja njiani, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufuata kokote utakakokwenda.”
58 Yesu akamwambia, “Mbweha wana mapango na ndege wa angani wana viota. Lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”
59 Yesu akamwambia mtu mwingine, “Nifuate!”
Lakini mtu yule akamwambia, “Bwana, niache nikamzike baba yangu kwanza.”
60 Lakini Yesu akamwambia, “Waache waliokufa wawazike wafu wao. Ni lazima uende kuhubiri kuhusu Ufalme wa Mungu.”
61 Mtu mwingine pia akamwambia, “Nitakufuata Bwana, lakini niruhusu kwanza nikaiage familia yangu.”
62 Yesu akamwambia, “Mtu yeyote anayeanza kulima, kisha akaangalia nyuma hajajiandaa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.”
Read full chapter
Luka 9:57-62
Neno: Bibilia Takatifu
Gharama Ya Kumfuata Yesu
57 Walipokuwa wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufu ata po pote utakapokwenda.” 58 Yesu akamwambia, “Mbweha wanaishi kwenye mapango yao na ndege kwenye viota vyao lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulala na kupumzika.”
59 Yesu alimwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.” 60 Yesu akamwam bia, “Waache wafu wawazike wafu wao. Bali wewe nenda ukautan gaze Ufalme wa Mungu.” 61 Mtu mwingine akamwambia, “Bwana nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.” 62 Yesu akamwambia, “Mtu ye yote ashikaye jembe kuanza kulima kisha akawa anageuka kutazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.” Yesu Awatuma Wafuasi Sabini na Wawili
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica