Yesu alipomaliza kuwaambia watu mambo haya alikwenda Kaper naumu. Huko mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi ambaye bwana wake alimpenda, alikuwa mgonjwa sana, karibu ya kufa. Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu aliwatuma wazee wa Kiyahudi wakam wombe aje kumponya mtumishi wake. Wale wazee walipofika kwa Yesu walimsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili msaada wako kwani yeye analipenda taifa letu, tena ametujengea sinagogi.”

Hivyo Yesu akaongozana nao. Hata alipoikaribia nyumba yake, yule jemadari aliwatuma rafiki zake, kumwambia Yesu, “Bwana, usijisumbue kuingia nyumbani kwangu. Sistahili heshima kubwa kiasi hicho, wala sikuona ninastahili mimi kuja kukuona binafsi. Sema neno moja tu na mtumishi wangu atapona. Katika nafasi yangu ya kazi nina wakubwa wangu na wapo askari wengine chini ya mamlaka yangu. Nikitoa amri kwa askari, ‘Nenda!’ huenda; nikimwambia mwingine, ‘Njoo!’ huja; na nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hiki,’ hufanya.” Yesu aliposikia maneno haya alishangaa sana. Akawageukia wale watu walioongozana naye aka waambia, “Hata katika Israeli yote sijakutana na mtu mwenye imani kama hii.” 10 Na wale waliotumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani kwa yule jemadari walikuta yule mtumishi amepona kabisa.

Read full chapter