Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima

Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda mizabibu katika shamba lake, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10 Wakati wa mavuno akamtuma mtumishi kwa hao wakulima aliowakodisha shamba ili wampatie sehemu ya mavuno. Lakini wale wakulima wakampiga na kumfukuza mikono mitupu. 11 Akamtuma mtumishi mwingine; naye pia wakam piga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12 Akampeleka wa tatu; wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.

13 “Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu nimpendaye, bila shaka yeye watamhesh imu.’ 14 Lakini wale wakulima walipomwona, wakashauriana, ‘Huyu ndiye mrithi, hebu tumwue ili sisi turithi hili shamba.’ 15 Kwa hiyo wakamtoa nje ya shamba, wakamwua.” Ndipo Yesu akauliza, “Sasa yule mwenye shamba atawafanyia nini wakulima hawa?

16 Atakuja awaue awapatie watu wengine shamba hilo.” Watu waliposikia hayo wakasema, “Jambo hili lisi tokee!”

17 Lakini Yesu akawakazia macho akasema, “Basi ni nini maana ya maandiko haya, ‘Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe la msingi.’

18 “Kila aangukaye kwenye jiwe hilo atakatika vipande vipande, na ye yote ambaye litamwangukia atasagika sagika.”

19 Waalimu wa sheria na wakuu wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja kwa sababu walifahamu kwamba huo mfano aliou toa uliwahusu wao. Lakini waliwaogopa watu.

Read full chapter