Luka 12:2-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Kila kitu kilichofichwa kitawekwa wazi, na kila kitu kilicho sirini kitajulikana. 3 Mnachokisema sirini kitasemwa mbele za watu. Na mliyonong'onezana katika vyumba vyenu, yatahubiriwa sehemu za wazi ambako kila mtu atasikia.”
Mwogopeni Mungu, Siyo Watu
(Mt 10:28-31)
4 Kisha Yesu akawaambia watu, “Ninawaambia ninyi, rafiki zangu, msiwaogope watu. Wanaweza kuua mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya chochote cha kuwaumiza. 5 Mwogopeni Mungu maana Yeye ndiye mwenye nguvu ya kuwaua na kuwatupa Jehanamu. Ndiyo, mnapaswa kumwogopa yeye.
6 Ndege wanapouzwa, ndege watano wadogo wanagharimu senti mbili tu za shaba. Lakini Mungu hasahau hata mmoja wao. 7 Ndiyo, Mungu anajua hata idadi ya nywele mlizonazo kwenye vichwa vyenu. Msiogope ninyi ni wa thamani kuliko ndege wengi.
Read full chapter© 2017 Bible League International