Luka 2:22-38
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Apelekwa Hekaluni
22 Baada ya kutimia kwa muda wa utakaso wa Yusufu na Mar iamu, kwa mujibu wa sheria ya Musa, walimpeleka mtoto Yerusalemu, wakamtoa kwa Bwana 23 kama ilivyotakiwa na sheria ya Bwana -“Kila mtoto wa kiume wa kwanza atakabidhiwa kwa Bwana.” 24 Pia walitoa sadaka, kama ilivyotakiwa na sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.” 25 Na alikuwepo huko Yerusalemu mzee mmoja jina lake Simeoni ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Siku zote alikuwa akitarajia ukombozi wa Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Pia Roho Mtaka tifu alikuwa amemhakikishia kuwa hangekufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Kwa hiyo, akiwa ameongozwa na Roho Mtaka tifu, Simeoni alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto mikononi mwake akamshukuru Mungu akisema: 29 “Sasa Bwana, niruhusu mimi mtumishi wako niende kwa amani kama ulivyoniahidi, 30 kwa sababu macho yangu yameuona wokovu 31 ulioandaa mbele ya watu wote, 32 nuru itakayowaangazia watu wa mataifa na kuleta utukufu kwa watu wako Israeli.” 33 Wazazi wa mtoto walistaajabu kwa yale yaliyokuwa yakisemwa kumhusu mtoto wao. 34 Simeoni akawabariki. Kisha akamwambia Mariamu, mama yake, “Mtoto huyu amechaguliwa na Mungu kwa makusudi ya kuanga mizwa na kuokolewa kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ya onyo kutoka kwa Mungu ambayo watu wengi wataikataa 35 ili kudhi hirisha mawazo yao ya ndani. Na uchungu kama kisu kikali utaku choma moyoni.” 36-37 ,Tena, alikuwepo Hekaluni nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti wa Fanueli, wa kabila la Asheri. Nabii Ana alikuwa mjane wa miaka themanini na minne naye alikuwa ameolewa kwa miaka saba tu mumewe akafariki. Yeye aliishi humo Hekaluni daima, akimwabudu Mungu na kuomba na kufunga.
38 Wakati huo huo, Ana alikuja mbele akamshukuru Mungu na kueleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica