Luka 9-13
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Awatuma Wanafunzi Kumi Na wawili
9 Yesu akawaita pamoja wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapa mamlaka na uwezo wa kufukuza pepo wote na kuponya magonjwa yote. 2 Kisha akawatuma waende wakautangaze Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
3 Akawaagiza akisema, “Msichukue cho chote safarini, wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha; na msichukue nguo za kubadili. 4 Mkikaribishwa katika nyumba yo yote muwe wageni wa nyumba hiyo hadi mtakapoondoka katika kijiji hicho. 5 Po pote ambapo hamtakaribishwa, mnapoondoka kung’uteni mavumbi miguuni mwenu kama ishara ya hukumu ya Mungu juu yao.”
6 Wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji wakihubiri Habari Njema na kuponya wagonjwa. 7 Habari zil imfikia Herode mtawala wa Galilaya kuhusu miujiza iliyokuwa iki fanyika, naye akafadhaika kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka!” 8 Wengine wakasema, “Ni Eliya ametutokea” na wengine kwamba, “Mmoja wa manabii wa kale amefufuka.” 9 Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa, ni nani huyu anayefanya maajabu haya ninayoambiwa?” Akajaribu sana amwone Yesu.
Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
10 Wanafunzi waliporudi walimweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua wakaenda peke yao mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida. 11 Lakini watu wengi wakafahamu alipokwenda, wakamfuata. Akawa karibisha, akawafundisha tena kuhusu Ufalme wa mbinguni na akapo nya wangonjwa. 12 Ilipokaribia jioni, wale wanafunzi kumi na wawili wakamwambia Yesu, “Waruhusu watu hawa waondoke ili waweze kujitafutia chakula na mahali pa kulala katika vijiji na mashamba ya jirani kwa maana hapa tuko nyikani.” 13 Akawajibu, “Wapeni chakula.” Wakasema, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili. Unataka tukanunue chakula cha kuwatosha watu wote hawa?” 14 Kwa kuwa walikuwapo wanaume wapatao elfu tano! Lakini Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini-hamsini.” 15 Wakawaketisha wote. 16 Yesu akaichukua mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavi bariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. 17 Kila mtu akala na kutosheka na vilipokusanywa vipande vilivyobaki, vilijaa vikapu kumi na viwili.
Petro Amkiri Bwana Yesu Kuwa Ndiye Kristo
18 Siku moja Yesu alipokuwa akisali faraghani akiwa na wana funzi wake aliwauliza, “Watu husema mimi ni nani?” 19 Wakam wambia, “Watu husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni nabii wa kale aliyefufuka kutoka kwa wafu.”
20 Kisha akawauliza, “Ninyi je, mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, “Wewe ndiye Kristo wa Mungu.” 21 Yesu akawaka taza wasimwambie mtu jambo hilo 22 akisema, “Imenipasa mimi Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, maku hani wakuu na walimu wa sheria. Nitauawa na siku ya tatu nitafuf uliwa.” 23 Kisha akawaambia wote, “Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane nafsi yake, achukue msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa maana ye yote atakayeshughulikia zaidi usalama wa nafsi yake ataipoteza. Lakini ye yote atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataisalimisha. 25 Je, kuna faida gani kwa mtu kuupata ulimwengu mzima ambapo kwa kufanya hivyo ataipoteza nafsi yake? 26 Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu, na mimi Mwana wa Adamu nitamwonea aibu mtu huyo nitakapo kuja katika utukufu wangu na wa Baba na wa malaika watakatifu. 27 Ninawaambia kweli, baadhi ya watu waliosimama hapa hawatakufa mpaka watakapouona Ufalme wa Mungu.”
Bwana Yesu Abadilika Sura
28 Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu alikwenda kusali mlimani pamoja na Petro, Yakobo na Yohana. 29 Alipokuwa akiomba, sura yake ili badilika, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta na kung’aa. 30 Ghafla wakawepo watu wawili wakaanza kuzungumza naye. Walikuwa ni Musa na Eliya! 31 Nao walionekana katika utukufu wakizungumza na Yesu kuhusu kifo chake ambacho kingetokea Yerusalemu.
32 Petro na wenzake ambao walikuwa wamelala usingizi mzito waliamka wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Musa na Eliya walipoanza kuondoka, Petro akamwambia Yesu, “Bwana ni vizuri mno kwamba tuko hapa! Tutajenga vibanda vitatu - kimoja chako, kingine cha Musa na kin gine cha Eliya.” Lakini Petro hakujua anasema nini. 34 Petro alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu kubwa na kivuli chake kikawafunika, na wale wanafunzi wakashikwa na hofu lile wingu lilipowafikia. 35 Sauti ikatoka kwenye wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu niliyemchagua, msikilizeni yeye.” 36 Baada ya sauti hiyo kusema, alionekana Yesu peke yake. Wale wanafunzi wakakaa kimya na kwa wakati huo hawakumwambia mtu ye yote yale waliyoy aona.
37 Kesho yake aliposhuka kutoka mlimani alikutana na umati mkubwa wa watu. 38 Ghafla, mtu mmoja kati yao akapiga kelele akasema, “Mwalimu, tafadhali nakuomba umwangalie mtoto wangu, ni mwanangu wa pekee. 39 Mara kwa mara pepo humshika na kumfanya apige kelele kisha humwangusha na kumtia kifafa akatokwa na povu mdomoni. Anamtesa sana na hamwachii ila kwa shida. 40 Nimewaomba wanafunzi wako wamwondoe huyo pepo lakini wameshindwa.” 41 Yesu akajibu, “Enyi watu mliopotoka, msio na imani, nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”
42 Yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo akamwangusha, akam tia kifafa. Lakini Yesu akamwamuru yule pepo amtoke. Akamponya yule mtoto akamkabidhi kwa baba yake. 43 Watu wote walishangaa walipoona huo uweza mkuu wa Mungu. Wakati watu walipokuwa wanas taajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye aliwaambia wanafunzi wake: 44 “ Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kuwekwa mikononi mwa wanadamu.” 45 Lakini wanafunzi wake hawakuyaelewa maneno hayo. Maana ya maneno hayo ilikuwa imefichwa ili wasiweze kuelewa, nao waliogopa kumwuliza.
Yesu Afundisha Kuhusu Ukubwa
46 Wanafunzi wakaanza kubishana wao kwa wao kuhusu nani kati yao alikuwa mkuu zaidi. 47 Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao, akamsimamisha mtoto mdogo karibu naye 48 kisha akawaambia, “Ye yote atakayemkaribisha mtoto huyu mdogo kwa jina langu atakuwa amenikaribisha; na ye yote atakayenikaribisha mimi atakuwa amem karibisha yeye aliyenituma; kwa maana yeye aliye mdogo kati yenu, ndiye aliye mkubwa kuliko wote.” 49 Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako tukamzuia kwa maana yeye si mmoja wetu.” 50 Yesu akasema, “Msimzuie kwa sababu ye yote ambaye hapingani nanyi, yuko upande wenu.”
Yesu Akataliwa Samaria
51 Siku zake za kurudi mbinguni zilipokaribia, Yesu aliamua kwamba lazima aende Yerusalemu na akaanza safari kuelekea huko. 52 Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu. 53 Lakini watu wa kijiji hicho walikataa kumpokea kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba ali kuwa anakwenda Yerusalemu. 54 Basi wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, wakasema: “Bwana, unataka tuamuru moto kutoka mbinguni uwaangamize?” 55 Yesu akageuka, akawakemea. 56 Wakaenda kijiji kingine.
Gharama Ya Kumfuata Yesu
57 Walipokuwa wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufu ata po pote utakapokwenda.” 58 Yesu akamwambia, “Mbweha wanaishi kwenye mapango yao na ndege kwenye viota vyao lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulala na kupumzika.”
59 Yesu alimwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.” 60 Yesu akamwam bia, “Waache wafu wawazike wafu wao. Bali wewe nenda ukautan gaze Ufalme wa Mungu.” 61 Mtu mwingine akamwambia, “Bwana nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.” 62 Yesu akamwambia, “Mtu ye yote ashikaye jembe kuanza kulima kisha akawa anageuka kutazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.” Yesu Awatuma Wafuasi Sabini na Wawili
10 Baada ya hayo, Yesu akawachagua wafuasi wengine sabini na wawili akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi lakini wafanya kazi ni wachache, kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno awapeleke wavunaji zaidi katika shamba lake. 3 Haya, nendeni. Ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. 4 Msichukue mkoba wala mfuko, wala viatu; na msipoteze muda kumsalimu mtu ye yote njiani. 5 Mkiingia nyumba yo yote kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ 6 Kama aishiye humo ni mwenye kupenda amani basi baraka hiyo itakaa naye, la sivyo, itawarudia. 7 Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa kile watakachowapa kwa sababu kila mfany akazi anastahili kulipwa mshahara. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba. 8 Mkienda katika mji mkapokelewa: kuleni mtakachoandal iwa; 9 waponyeni wagonjwa na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu.’
10 “Lakini mkiingia katika mji msikaribishwe, nendeni katika mitaa yake mkaseme: 11 ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoko miguuni mwetu tunayakung’uta juu yenu; lakini fahamuni ya kwamba Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu!’ 12 “Nawahakikishia kwamba siku ile Mungu atakapouhukumu ulimwengu adhabu ya Sodoma itakuwa nafuu kuliko ya mji huo! 13 Ole wenu watu wa Korazini na wa Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifany ika Tiro na Sidoni watu wa huko wangalitubu zamani, wakivaa magu nia na kujimwagia majivu kama dalili ya majuto. 14 Lakini siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko kwenu. 15 Na ninyi je, watu wa Kapernaumu, mnafikiri mtainuliwa juu hadi mbinguni? La, Mungu atawatupa chini hadi kuzimuni. 16 “Ye yote atakayewasikiliza ninyi amenisikiliza mimi, naye awakataaye amenikataa. Lakini anikataaye mimi amemkataa yeye aliyenituma.”
17 Wale wanafunzi sabini na wawili wakarudi wakiwa na furaha. Wakamwambia Yesu, “Bwana, tukilitumia jina lako, hata pepo wanatutii!” 18 Akawajibu, “Nimemwona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni. 19 Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru. 20 Lakini msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii, ila furahini kwa kuwa majina yenu yamean dikwa mbinguni.”
21 Wakati huo, Yesu akiwa amejawa na furaha ya Roho Mtaka tifu, akasema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya ambayo umewaficha wenye elimu na wenye hekima umependa kuwafunulia wale wakuaminio kama watoto wadogo. Na haya yote yamefanyika kwa mapenzi yako Baba. 22 Baba yangu amenika bidhi mambo yote. Hakuna anayemfahamu Mwana isipokuwa Baba: na hakuna anayemfahamu Baba isipokuwa Mwana na wale ambao Mwana ame penda humdhihirisha Baba kwao.” 23 Basi Yesu akawageukia wana funzi wake akawaambia faraghani, “Mmebarikiwa kuona mambo haya mnayoyaona! 24 Nawaambie ni kweli, manabii wengi na wafalme wal itamani kuona mnayoyaona na kusikia mnayoyasikia lakini hawaku pata nafasi hiyo.” Mfano Wa Msamaria Mwema
25 Mwalimu mmoja wa sheria alisimama akajaribu kumpima Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” 26 Yesu akamjibu, “Sheria inasemaje? Unaitafsiri vipi?” 27 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.” 28 Yesu akamwambia, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29 Lakini yule mwalimu wa sheria akitaka kuon yesha kwamba hoja yake ilikuwa na maana zaidi, akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja aliteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njiani akashambuliwa na majambazi; wakamwibia kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga wakamwacha karibu ya kufa. 31 litokea kwamba kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile. Ali pomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. 32 Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.
33 “Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomkuta, alimwonea huruma, 34 akamwendea akasafisha maj eraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. 35 Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.
36 “Unadhani ni yupi kati ya hawa watatu alikuwa jirani yake yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi?”
37 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akasema, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”
Yesu Awatembelea Martha na Mariamu
38 Wakati Yesu na Wanafunzi wake walipokuwa wakiendelea na safari yao ya kwenda Yerusalemu, walifika katika kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha Yesu nyum bani kwake. 39 Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Mariamu ambaye aliketi chini karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.
40 Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote. Kwa hiyo alikuja kwa Yesu akalalamika, “Bwana, hujali kwamba mdogo wangu ameniachia kazi zote? Mwambie aje anisaidie!” 41 Bwana akamjibu, “Martha! Martha! Mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 42 Unahitaji kujua kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kil icho bora, na hakuna mtu atakayemnyang’anya.” Yesu Awafundisha Wanafunzi Wake Kuomba
11 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomal iza, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tafadhali tufundishe kuomba kama Yohana Mbatizaji alivyowafundisha wana funzi wake.” 2 Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. 3 Utupatie chakula chetu kila siku. 4 Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.” 5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6 Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ 7 Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ 8 “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji. 9 Kwa hiyo nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. 10 Kwa kuwa kila anayeomba hupewa; naye atafutaye, hupata; na kila abishaye, hufunguliwa mlango. 11 “Ni baba yupi miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12 Au akimwomba yai atampa nge? 13 Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho
Yesu Na Beelzebuli
14 Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa. 15 Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.” 16 Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
17 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia. 18 Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. 19 Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia. 20 Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia. 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama. 22 Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote. 23 “Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.
24 “Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’ 25 Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri, 26 huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”
27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.” 28 Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”
Ishara Ya Yona
29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu aliendelea kufundisha akisema, “Watu wa kizazi hiki ni waovu. Wanatafuta ishara lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 30 Kwa maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo mimi Mwana wa Adamu nitakavyokuwa ishara kwa kizazi cha sasa. 31 Siku ya hukumu malkia wa Sheba atashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani. Lakini sasa, aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa. 32 Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu Yona ali powahubiria waliacha dhambi zao. Lakini sasa aliye mkuu kuliko
Taa Ya Mwili
33 “Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake. 34 Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza. 35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza. 36 Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”
Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria
37 Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja. 38 Farisayo yule alipoona kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula alishangaa. 39 Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu. 40 Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia? 41 Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.
42 “Lakini ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnamtolea Mungu sehemu ya kumi ya mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu. Mngeweza kutoa matoleo hayo pasipo kusahau haki na upendo kwa Mungu.
43 “Ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni! 44 Ole wenu! Kwa maana ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”
45 Mwalimu mmoja wa sheria akasema, “Mwalimu, unapozungumza hivyo unatushutumu na sisi wanasheria!” 46 Yesu akamjibu, “Hata ninyi wanasheria, ole wenu! Mnawabebesha watu mzigo wa sheria ambazo hawawezi kuzitimiza; wala hamfanyi lo lote kuwa saidia iwe rahisi kwao kuzitimiza. 47 Ole wenu kwa kuwa mnawa jengea makaburi manabii waliouawa na babu zenu. 48 Kwa kufanya hivyo mnakiri kwamba mnaunga mkono kitendo hicho walichofanya babu zenu. Wao waliua na ninyi mnatengeneza makaburi.
49 “Ndio maana Mungu katika hekima yake alisema, ‘Nita wapeleka manabii na mitume, na baadhi yao watawaua na wengine watawatesa.’ 50 Kwa hiyo damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa dunia itahesabiwa juu ya watu wa kizazi hiki; 51 tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Nawaambia kweli, watu wa kizazi hiki wataadhibiwa kwa ajili yao wote. 52 Ole wenu ninyi wanashe ria kwa maana mmeuchukua ufunguo unaofungua nyumba ya maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”
53 Yesu alipoondoka hapo, walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanampinga vikali na kumwuliza maswali mengi, 54 wakijar ibu kumtega ili aseme kitu ambacho watakitumia kumshitaki.
Yesu Awaonya Na Kuwafariji Wanafunzi
12 Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.
2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi. 5 Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kumwua mtu ana mamlaka ya kumtupa motoni. Naam: huyo, mwogopeni! 6 Mnajua kwamba mbayuwayu watano huuzwa kwa bei ndogo sana. Lakini Mungu anamjali kila mmoja wao. 7 Mungu anafahamu hata idadi ya nywele zilizoko katika vichwa vyenu. Kwa hiyo msiogope: ninyi mna thamani zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 8 “Ninawaambia, kila atakayenikiri mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkiri mbele ya malaika wa Mungu. 9 Lakini kila anayenikana mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkana mbele ya malaika wa Mungu. 10 Na kila atakayesema neno baya kunihusu mimi Mwana wa Adamu atasamehewa. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. 11 “Na watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12 kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”
Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”
13 Na mtu mmoja katika umati akasema, “Bwana, mwambie ndugu yangu anigawie urithi aliotuachia baba yetu.” 14 Yesu akamwam bia, Rafiki, ni nani aliyenifanya mimi niwe hakimu wenu au mga wanyaji wa urithi wenu?” 15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”
16 Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’ 18 Kisha akasema, ‘Nitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Na nitasema moy oni, ‘Hakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.’ 20 Lakini Mungu akamwambia, ‘Mjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?’ 21 Hivi ndivyo itakavy okuwa kwa mtu ye yote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.”
22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo ninawaambia, msihangaikie maisha yenu, kwamba mtakula nini; au miili yenu kwamba mtavaa nini. 23 Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege! 25 Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja? 26 Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo; kwa nini basi mhangaikie hayo mengine? 27 Yata zameni maua yanavyostawi: hayafanyi kazi, wala kujitengenezea nguo; lakini ninawaambia, hata Sulemani katika ufahari wake wote, hakuwahi kuvishwa vizuri kama ua mojawapo! 28 Ikiwa Mungu huyav isha hivi majani ambayo leo yapo shambani na kesho yanachomwa moto; ataachaje kuwavisha ninyi hata zaidi? Mbona mna imani ndogo! 29 Wala msihangaike mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. 30 Watu wasiomjua Mungu huhan gaika sana juu ya vitu hivi. Lakini Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnavihitaji. 31 Basi, tafuteni Ufalme wa Mungu; na hivyo vyote atawapatia.”
32 “Ninyi kundi dogo, msiogope kwa maana Mungu amependa mtawale naye katika ufalme wake. 33 Uzeni mali zenu muwape mas kini; ili mjipatie mikoba isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbin guni ambapo mwizi hafiki wala nondo haharibu. 34 Kwa maana unapoiweka akiba yako ndipo na moyo wako utakapokuwa.”
Kukesha
35 “Muwe tayari mkiwa mmevaa, na taa zenu zikiwaka. 36 Muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka haru sini, ili atakapokuja na kugonga mlango wamfungulie mara moja. 37 Itakuwa ni heri kwa wale watumishi ambao bwana wao akija ata wakuta wanamngoja. Nawaambieni kweli, atajiandaa na kuwaketisha karamuni awahudumie. 38 Itakuwa ni furaha kubwa kwao ikiwa ata wakuta tayari hata kama atakuja usiku wa manane au alfajiri.
39 Fahamuni kwamba kama mwenye nyumba angalijua ni saa ngapi mwizi atakuja, angalijiandaa asiiachie nyumba yake ivunjwe. 40 Kwa hiyo, ninyi pia mkae tayari, kwa maana mimi Mwana wa Adamu nita kuja saa ambayo hamnitegemei.”
Mtumishi Mwaminifu Na Asiye mwaminifu
41 Ndipo Petro akamwambia, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?” 42 Yesu akamwambia, “Ni yupi wakili mwaminifu na mwenye busara? Ni yule ambaye bwana wake atamfanya mtawala juu ya nyumba yake yote naye awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa. 43 Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44 Ninawahakikishia kwamba atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. 45 Lakini kwa mfano, kama yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anachelewa kurudi,’ halafu aanze kuwa piga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa, 46 bwana wake atarudi siku ambayo hakumtazamia, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamwadhibu vikali pamoja na wote wasiotii. 47 Na mtumishi ambaye anafahamu mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, pia ataad hibiwa vikali. 48 Lakini mtumishi ambaye hafahamu anachotakiwa kufanya na akafanya kitu kinachostahili adhabu, atapata adhabu ndogo. Mungu atatarajia vingi kutoka kwa mtu aliyepewa vipawa vingi; na mtu aliyekabidhiwa vingi zaidi, atadaiwa zaidi pia.”
49 “Nimekuja kuleta moto duniani! Laiti kama dunia inge kuwa tayari imeshawaka! 50 Lakini kuna ubatizo ambao lazima niu pokee na dhiki yangu ni kuu mpaka ubatizo huo utakapokamilika.
51 “Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambieni sivyo; nimekuja kuleta mafarakano. 52 Kuanzia sasa, katika nyumba ya watu watano kutakuwa na mgawanyiko: watatu wakipingana na wawili, na wawili wakipingana na watatu. 53 Baba atapingana na mwanae na mwana atapingana na babaye; mama atapingana na bin tiye na binti atapingana na mamaye; mama mkwe atapingana na mke wa mwanae ambaye naye atapingana na mama mkwe wake.”
Kutambua majira
54 Kisha Yesu akawaambia watu, “Mkiona wingu likitokea mag haribi, mara moja mnasema, ‘Mvua hiyo inakuja!’ na inakuwa hivyo. 55 Na mnapouona upepo wa kusi ukivuma, mnasema, ‘Kutakuwa na joto!’ Na linakuwepo. 56 Enyi wanafiki! Mnaweza kutambua dalili za hali ya hewa; kwa nini basi hamtambui maana ya mambo yanayoto kea sasa? 57 Kwa nini hamuamui lililo haki kutenda? 58 Kama mtu akikushtaki mahakamani, jitahidi sana kupatana na mshtaki wako wakati mkiwa mnaenda mahakamani, ili asikufikishe mbele ya hakimu, na hakimu akakukabidhi kwa polisi, na polisi wakakutia gerezani. 59 Nakuhakikishia kwamba, hutatoka huko gerezani mpaka umelipa faini yote.”
13 Wakati huo, watu fulani walimwambia Yesu habari za Wagali laya ambao Pilato aliwaua na damu yao akaichanganya na damu ya sadaka waliyokuwa wakimtolea Mungu. 2 Yesu akawajibu, “Mnadhani Wagalilaya hao walikufa kifo cha namna hiyo kwa kuwa walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 3 Sivyo hata kidogo. Ninyi pia msipoacha dhambi zenu mtaangamia vivyo hivyo. 4 Au wale watu kumi na wanane ambao walikufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu, mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu? 5 Nawaambieni, sivyo! Ninyi pia msipoacha dhambi zenu, mtaangamia vivyo hivyo.”
Mfano Wa Mti Usiozaa Matunda
6 Kisha Yesu akatoa mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaenda kutafuta tini kwenye mti huo asipate hata moja. 7 Kisha akamwambia mtunza shamba:, ‘Kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, sijawahi kupata hata moja. Ukate, sioni kwa nini uendelee kutumia ardhi bure!’ 8 Yule mtunza shamba akam jibu, ‘Bwana, tuuache tena kwa mwaka mmoja zaidi, niulimie, niuwekee mbolea. 9 Ukizaa matunda, vema; na usipozaa baada ya hapo, utaukata.”’ Yesu Amponya Mwanamke Siku Ya Sabato
10 Siku moja ya sabato, Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. 11 Na hapo alikuwapo mwanamke mmoja alikuwa ameugua kwa muda wa miaka kumi na minane kutokana na pepo ali yekuwa amemwingia. Hali hiyo ilimfanya mwanamke huyo apindike hata asiweze kusimama wima. 12 Yesu alipomwona, akamwita akam wambia, “Mama, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” 13 Yesu akamwekea mikono, na mara akasimama wima, akamtukuza Mungu. 14 Mkuu wa sinagogi akakasirika kwa kuwa Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya sabato. Kwa hiyo akawaambia watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi, katika siku hizo, njooni mpo nywe; msije kuponywa siku ya sabato!”
15 Lakini Bwana akamjibu, “Ninyi ni wanafiki! Kila mmoja wenu humfungulia ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya sabato. 16 Je, huyu mama, ambaye ni binti wa Ibrahimu aliyefungwa na shetani kwa miaka yote hii kumi na minane, hastahili kufunguliwa kutoka katika kifungo hicho siku ya sabato?” 17 Aliposema haya, wapinzani wake wakaona aibu lakini watu wakafurahi kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyoyafanya. Mfano Wa Punje Ya Haradali
18 Kisha Yesu akauliza, “Ufalme wa Mungu ukoje? Nitaufanan isha na nini? 19 Umefanana na punje ndogo sana ya haradali ambayo mtu aliichukua akaipanda katika shamba lake, ikamea, ikawa mti na ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”
Mfano Wa Hamira
20 Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha na nini Ufalme wa Mungu? 21 Uko kama hamira ambayo mwanamke aliichukua na kuichan ganya kwenye vipimo vitatu vya unga wa ngano na wote ukaumuka.”
Mlango Mwembamba
22 Yesu akapita katika miji na vijiji akifundisha wakati akisafiri kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” 24 Akajibu, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana, nawaambia, wengi watataka kuingia na hawataweza. 25 Wakati mwenye nyumba ataka poamka na kufunga mlango, mtasimama nje mkigonga mlango na kusema, ‘Bwana utufungulie!’ Atawajibu, ‘Sijui mtokako!’ 26 Nanyi mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, ulifundisha katika mitaa yetu!’ 27 Lakini yeye atawajibu, ‘Sijui mtokako. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’ 28 Ndipo kutakuwapo na kilio na kusaga meno mtakapomwona Ibrahimu, Isaka na Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, wakati ninyi mkiwa mmetupwa nje. 29 Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi na kaskazini na kusini na wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa kar amuni katika Ufalme wa Mungu. 30 Hakika wapo watu ambao sasa wako mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wengine walio wa kwanza sasa watakaokuwa wa mwisho.” Yesu Aomboleza Juu Ya Yerusalemu
31 Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” 32 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie yule mbweha: ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa leo na kesho, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu. 33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa, kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.
Copyright © 1989 by Biblica