39 Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Huyu mtu hawezi kuwa ni nabii. Kama ange kuwa nabii angetambua kuwa huyu mwanamke ni kahaba.” 40 Kisha Yesu akijua mawazo ya yule Farisayo akamwambia, “Simoni, kuna jambo nataka kukuambia.” Simoni akajibu “Sema, mwalimu.” 41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: mmoja shillingi elfu tano na mwingine shillingi mia tano.

Read full chapter