Bwana Wa Sabato

Siku moja ya sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke ya ngano, wakayafi kicha na kula punje zake. Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnavunja sheria kwa kuvuna ngano siku ya sabato?”

Yesu akawajibu, “Ninyi hamsomi Maandiko? Hamjasoma alicho fanya Mfalme Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? Aliingia Hekaluni, akachukua ile mikate ya madhabahuni -ambayo huliwa na makuhani peke yao -akala, kisha akawapa na wafuasi wake wakala!” Akaongezea kusema, “Mimi Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”

Ikawa siku nyingine ya sabato Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi, na alikuwepo mtu ambaye mkono wake wa kuume uli kuwa umepooza. Walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanangoja waone kama atamponya mtu siku ya sabato ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Kwa hiyo akamwam bia yule aliyepooza mkono, ’Njoo usimame hapa mbele ili kila mtu akuone.” Yule mtu akaja mbele. Kisha Yesu akawageukia wale walimu wa sheria na Mafarisayo akasema, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya sabato - kutenda mema au kutenda mabaya? Kuokoa maisha au kuyaangamiza?” 10 Akawatazama watu wote waliokuwepo. Kisha akamwambia yule aliyepooza mkono, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha na mkono wake ukapona kabisa! 11 Wale wakuu wakakasirika sana. Wakaanza kushauriana, “Tumfa nye nini huyu Yesu?’ ’

Kuchaguliwa Kwa Mitume Kumi Na Wawili

12 Siku moja Yesu alikwenda milimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 13 Asubuhi akawaita wanafunzi wake, na kati yao akachagua kumi na wawili akawapa cheo cha “mitume.” Majina yao ni haya: 14 Simoni, aliyemwita Petro; Andrea, nduguye Simoni; Yakobo; Yohana; Filipo; Bartholomayo; 15 Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Simoni, aliyeitwa Mzalendo; 16 Yuda, mwana wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ambaye baadaye alimsaliti Yesu.

Yesu Aponya Wengi

17 Akashuka pamoja nao akasimama mahali penye uwanja tambar are. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu waliotoka sehemu zote za Yudea na Yerusalemu na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walikuwa wamekuja kumsiki liza na kuponywa magonjwa yao. 18 Hata wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu nao walimjia akawaponya. 19 Na watu wote wali kuwa wanajitahidi kumgusa kwa maana walipofanya hivyo, nguvu zil ikuwa zikimtoka na kuwaponya wote.

20 Kisha akawatazama wanafunzi wake akasema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini kwa sababu Ufalme wa mbinguni ni wenu! 21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa! Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka. 22 Mmebari kiwa ninyi watu watakapowachukia na kuwakataa na kuwatukana na kuharibu sifa yenu kwa ajili yangu. 23 Yatakapotokea haya fura hini na kuruka ruka kwa furaha kwa sababu zawadi kubwa imewekwa mbinguni kwa ajili yenu. Hata baba zao waliwatendea manabii wa zamani vivyo hivyo.

24 “Lakini ole wenu ninyi matajiri, kwa sababu mmekwisha pata furaha yenu! Ole wenu ninyi mlioshiba, maana mtaona njaa! 25 Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, maana mtalia na kuomboleza! 26 Ole wenu mtakaposifiwa na watu, kwani ndivyo baba zao walivy owasifu manabii wa uongo.”

Wapendeni Adui Zenu

27 “Sikieni niwaambie, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 28 Wabarikini wanaowalaani, waombeeni mema wanaowaumiza. 29 Mtu akikupiga kofi, mgeuzie na shavu la pili. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua na shati lako pia. 30 Aombae mpe, na mtu akichukua mali yako usidai urudishiwe. 31 Watendee wengine unavyopenda nao wakutendee. 32 Je, kuna sifa gani mnapowapenda watu wawapendao? Hata wasiomjua Mungu huwapenda wawapendao. 33 Tena kuna sifa gani mnapowatendea mema wale wanaowatendea mema? Hata wasiomjua Mungu hufanyiana hivyo. 34 Tena mnapowakopesha wale tu ambao mnategemea kuwa watawalipa, kuna sifa gani? Hata watu wasiomjua Mungu huwakopesha wenye dhambi wenzao wakiwa na hakika ya kurudishiwa mali yao yote. 35 Bali, wapendeni adui zenu, watendeeni mema. Wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo mtapata zawadi kubwa nanyi mtakuwa wana wa Mungu Aliye Juu. Yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na watu waovu. 36 Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.”

Msiwahukumu Wengine

37 “Msiwahukumu wengine nanyi hamtahukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa. 38 Muwe wepesi wa kutoa nanyi mtapokea. Kipimo mtakachotoa mtar udishiwa kikiwa kimejaa na kushindiliwa na kutikiswa na kufurika. Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.”

Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.”

39 Pia akawapa mfano akasema, “Je, kipofu anaweza kumwon goza kipofu mwenzake? Si wote wawili watatumbukia shimoni? 40 Mwanafunzi hawezi kuwa mjuzi kuliko mwalimu wake, ila akihi timu, anaweza kuwa bingwa kama mwalimu wake. 41 Mbona unatazama sana kipande kilichoko katika jicho la mwenzako nawe huoni pande lililoko ndani ya jicho lako? 42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, hebu, nikusaidie kutoa kipande hicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni pande hilo lililoko ndani ya jicho lako? Mnafiki wewe! Ondoa kwanza pande hilo ndani ya jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kuondoa kipande kili choko ndani ya jicho la ndugu yako.

43 “Hakuna mti bora uzaao matunda hafifu wala hakuna mti hafifu uzaao matunda bora. 44 Kila mti hutambuliwa kwa matunda yake. Tini hazichumwi kwenye michongoma wala zabibu hazichumwi kwenye majani mwitu. 45 Hali kadhalika mtu mwema hutambulikana kwa matendo yake mazuri yatokayo katika moyo mwema. Mtu mwovu pia hutenda maovu yatokanayo na uovu uliojaa ndani ya moyo wake. Mtu hunena yale yaliyojaa moyoni mwake.

46 “Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana’ nanyi hamfanyi ninay owaambia?

47 Nitawaambieni alivyo mtu anayesikia na kufanya ninay osema. 48 Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba akachimba chini na kujenga msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipotokea, yakaikumba ile nyumba wala haikutikisika, kwani ilikuwa na msingi imara. 49 Lakini yeye ayasikiaye maneno yangu na asiyafuate, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya mchanga bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ilianguka mara, na kuporomoka kabisa.”