36 Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.”

Msiwahukumu Wengine

37 “Msiwahukumu wengine nanyi hamtahukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa. 38 Muwe wepesi wa kutoa nanyi mtapokea. Kipimo mtakachotoa mtar udishiwa kikiwa kimejaa na kushindiliwa na kutikiswa na kufurika. Kwa kuwa jinsi mtakavyotoa, ndivyo mtakavyopata.”

Read full chapter