Siku moja Yesu alipokuwa amesimama akihubiri karibu na ziwa la Genesareti, watu wengi walimsonga ili wapate kusikia neno la Mungu. Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, lakini wenye mashua walikuwa wakiosha nyavu zao. Akaingia katika mashua moja, akamwomba mwenye mashua, ambaye jina lake lilikuwa Simoni, aisogeze zaidi katika maji. Kisha akakaa kwenye mashua, akaanza kuwafundisha.

Alipokwisha zungumza na watu akamwambia Simoni, “Sasa ipe leke mashua hadi mahali penye kina kirefu, kisha mshushe nyavu zenu nanyi mtapata samaki.”

Simoni akamjibu, “Bwana, tumekesha usiku kucha tukivua na hatukuambulia kitu cho chote. Lakini, kwa kuwa wewe umesema, tutazishusha nyavu.” Nao walipofanya kama Yesu alivyowaagiza, nyavu zao zikajaa samaki, zikaanza kuchanika! Wakawaashiria wavuvi wa ile mashua nyingine waje kuwasaidia. Mashua zote mbili zikajaa samaki hata karibu kuzama.

Simoni Petro alipoona yaliyotokea alipiga magoti mbele ya Yesu akamwambia, “Bwana,tafadhali uniache kwa maana mimi ni mwe nye dhambi.” Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wamesh angazwa sana na wingi wa samaki waliopata. 10 Hali kadhalika wavuvi wa ile mashua nyingine, Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo walishangazwa pia. Ndipo Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.”

11 Nao walipokwisha fikisha mashua yao nchi kavu, wakaacha vyote, wakamfuata Yesu. Yesu Amponya Mwenye Ukoma

12 Siku moja Yesu alipokuwa katika mji fulani alitokea mtu mwenye ukoma mwili mzima. Alipomwona Yesu alijitupa chini kwa kunyenyekea akamsihi akisema, “Bwana, ukitaka unaweza kunita kasa!” 13 Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Ndio, nataka upone; takasika!” Wakati huo huo, ukoma wote ukamtoka . 14 Yesu akamwambia, “Usimweleze mtu ye yote jinsi ulivyopata kupona bali nenda moja kwa moja hadi kwa kuhani ili aone kuwa kweli umepona. Kisha utoe sadaka ya shukrani, kama she ria ya Musa inavyoagiza, ili kuthibitisha kuwa umetakasika.”

15 Lakini sifa za Yesu zikazidi sana kuenea. Watu wakamimi nika kwa wingi kutoka kila upande kuja kumsikiliza na kuponywa maradhi yao. 16 Ila mara kwa mara alitoka peke yake akaenda pasipo na watu akaomba.

Yesu Amponya Mwenye Kupooza

17 Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na wal imu wa sheria kutoka katika kila mji wa wilaya za Galilaya, Yudea na Yerusalemu walikuwepo. Na Yesu alikuwa amejaa nguvu ya Mungu ya kuponya wagonjwa.

18-19 Kisha wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwe nye kitanda. Wakajaribu kumpitisha ndani wamfikishe alipokuwa Yesu, lakini wakashindwa kwa sababu ya msongamano wa watu. Basi wakampandisha juu ya paa, wakaondoa baadhi ya vigae, wakapata nafasi ya kumteremsha yule mgonjwa pamoja na kitanda chake kwa kamba, hadi mbele ya Yesu. 20 Alipoona imani yao, Yesu alimwam bia yule mgonjwa, “Rafiki yangu, umesamehewa dhambi zako.” 21 Wale walimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kusemezana, “Mbona huyu anakufuru! Anadhani yeye ni nani? Hakuna awezae kusamehe dhambi ila Mungu peke yake.”

22 Yesu alifahamu mawazo yao kwa hiyo akawauliza, “Kwa nini mnafikiri mimi ninakufuru? 23 Je, ni lipi lililo rahisi zaidi, kumwambia huyu, ‘Umesamehewa dhambi zako’; au kusema, ‘Simama utembee?’ 24 Sasa nitawahakikishia kuwa mimi Mwana wa Adamu ninao uwezo wa kusamehe dhambi duniani.” Akamgeukia yule mgonjwa aliyepooza, akasema, “Nakuambia: Simama! Chukua kitanda chako uende nyumbani.” 25 Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu. 26 Wote waliokuwepo wakastaajabu sana. Wakajaa hofu. Wakamtukuza Mungu, wakasema, “Tumeona maajabu leo.”

Yesu Amwita Lawi

27 Baada ya haya Yesu alimwona afisa mmoja mtoza kodi jina lake Lawi akiwa ofisini mwake, akamwambia, “Njoo uwe mmoja wa wanafunzi wangu.” 28 Lawi akaacha vyote, akaondoka, akamfuata Yesu. 29 Baadaye Lawi akafanya karamu kubwa kumkaribisha Yesu nyumbani kwake. Watoza kodi wengi walikuwa miongoni mwa watu wal ioalikwa. 30 Basi baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria ambao walikuwa kundi moja wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu wakisema, “Mbona mnakula na kunywa na wenye dhambi?” 31 Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 32 Sikuja kwa ajili ya wenye haki bali nimekuja kuwaita wenye dhambi ili watubu.”

Yesu Aulizwa Habari Za Kufunga

33 Baadhi ya watu wakamwuliza Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na kusali mara kwa mara. Mbona wanafunzi wako wanakula na kunywa tu?”

34 Yesu akawajibu, “Je, inawezekana wageni walioalikwa har usini kufunga wakati wakiwa na Bwana Harusi? 35 Lakini wakati utafika ambapo Bwana Harusi ataondolewa. Wakati huo ndipo wataka pofunga.

36 Yesu akawapa mfano akawaambia: “Hakuna mtu anayechana nguo mpya ili apate kiraka cha kuweka kwenye nguo kuu kuu. Akifa nya hivyo ataharibu ile nguo mpya na ile kuu kuu itaonekana mbaya zaidi ikiwa na kiraka kipya. 37 Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vilivyochakaa; ukifanya hivyo, hivyo viriba vitapa suka na divai yote itamwagika. 38 Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 39 Na pia hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai iliyoiva vizuri. Kwa maana husema, ‘Hii divai iliyoiva siku nyingi ni bora zaidi.’ ”