Add parallel Print Page Options

26 Kila mtu alishangaa na kuanza kumsifu Mungu. Wakajawa na hofu kuu baada ya kuiona nguvu ya Mungu. Wakasema, “Leo tumeona mambo ya kushangaza!”

Lawi (Mathayo) Amfuata Yesu

(Mt 9:9-13; Mk 2:13-17)

27 Baada ya hayo Yesu alitoka nje akamwona mtoza ushuru amekaa sehemu yake ya kukusanyia ushuru. Jina lake aliitwa Lawi. Yesu akamwambia, “Nifuate!” 28 Lawi akasimama, akaacha kila kitu na kumfuata Yesu.

Read full chapter