26 Wote waliokuwepo wakastaajabu sana. Wakajaa hofu. Wakamtukuza Mungu, wakasema, “Tumeona maajabu leo.”

Yesu Amwita Lawi

27 Baada ya haya Yesu alimwona afisa mmoja mtoza kodi jina lake Lawi akiwa ofisini mwake, akamwambia, “Njoo uwe mmoja wa wanafunzi wangu.” 28 Lawi akaacha vyote, akaondoka, akamfuata Yesu.

Read full chapter