39 Basi Yesu akasimama kando ya kitanda chake akaiamuru ile homa imtoke. Homa ikamtoka yule mama. Akaamka mara moja akaanza kuwahudumia. 40 Jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwa Yesu. Akamgusa kila mgonjwa, akawaponya wote. 41 Pepo wachafu pia waliwatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walifahamu kuwa yeye ni Kristo.

Read full chapter