Yohana Mbatizaji Aanza Kuhubiri

Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Neno la Mungu lilimfikia Yohana mwana wa Zakaria alipokuwa nyikani. Wakati huo Pontio Pilato alikuwa mtawala wa Yudea; Her ode mtawala wa Galilaya, nduguye Filipo mtawala wa Iturea na Tra koniti; na Lisania alikuwa mtawala wa Abilene. Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu.

Yohana akazunguka sehemu zote za kando kando ya mto Yordani akihubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili wasamehewe dhambi zao. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aitae nyikani, ‘Mtayarishieni Bwana njia , nyoosheni sehemu zote atakazopita, jazeni kila bonde, sawazisheni milima yote. Na watu wote watamwona Mwokozi aliyetumwa na Mungu.’ ”

Yohana akawaambia wale waliokuja ili awabatize, “Enyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya muepuke hukumu ya Mungu ita kayokuja? Kama kweli mmetubu, basi onyesheni kwa matendo yenu. Wala msidhani kuwa mtasamehewa kwa kuwa ninyi ni uzao wa Ibra himu. Nawaambia wazi, Mungu anaweza kabisa kumpa Ibrahimu watoto kutoka katika haya mawe! Na hivi sasa hukumu ya Mungu, kama shoka kwenye shina la mti, iko juu yenu. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa katwa na kutupwa motoni.”

10 Watu wakamwuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?” 11 Aka waambia: “Aliye na nguo mbili amgawie asiye na nguo; kama una chakula wape wenye njaa.”

12 Watoza kodi nao pia walikuja ili wabatizwe; wakamwuliza, “Bwana, na sisi inatupasa tufanyeje?”

13 Akawajibu: “ Msimdhulumu mtu kwa kudai kodi zaidi ya ile iliyoamriwa.”

14 Na baadhi ya askari wakamwuliza, “Na sisi je, tufanye nini?” Akawajibu: “Msichukue fedha za watu kwa kutumia nguvu; msiwashtaki watu kwa kuwasingizia makosa; bali mtosheke na misha hara yenu!”

15 Siku hizo watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wakijiuliza mioyoni mwao kama Yohana ndiye Kristo.

16 Yohana aliwajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini anayekuja ni mkuu kuliko mimi, sistahili hata kuwa mtumwa wake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

17 “Yuko tayari na pepeto lake mkononi, tayari kusafisha mahali pake pa kukusanyia mazao. Nafaka safi ataiweka ghalani lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”

18 Yohana alitumia mifano mingine mingi kuwaonya watu na kuwatangazia Habari Njema. 19 Lakini Yohana alipomkanya Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia mke wa kaka yake, na maovu men gine aliyofanya, 20 Herode aliongezea uovu huo kwa kumfunga

Kubatizwa Kwa Bwana Yesu

21 Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. 22 Roho Mtakatifu akash uka juu yake kama hua; na sauti ikasikika kutoka mbinguni ikisema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa, ninapendezwa nawe.”

Ukoo Wa Bwana Yesu

23 Yesu alikuwa na umri wa miaka kama thelathini hivi ali poanza kazi ya kuhubiri. Yesu alijulikana kama mtoto wa Yusufu. Yusufu alikuwa mwana wa Eli, 24 Eli alikuwa mwana wa Mathati, Mathati alikuwa mwana wa Lawi, Lawi alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Yanai, Yanai alikuwa mwana wa Yusufu 25 Yusufu alikuwa mwana wa Matathia, Matathia alikuwa mwana wa Amosi, Amosi alikuwa mwana wa Nahumu, Nahumu alikuwa mwana wa Esli, Esli ali kuwa mwana wa Nagai, 26 Nagai alikuwa mwana wa Maathi, Maathi alikuwa mwana wa Matathia, Matathia alikuwa mwana wa Semeini, Semeini alikuwa mwana wa Yoseki, Yoseki alikuwa mwana wa Yoda, 27 Yoda alikuwa mwana wa Yoanani, Yoanani alikuwa mwana wa Resa, Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli, Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli, Shealtieli alikuwa mwana wa Neri, 28 Neri alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Adi, Adi alikuwa mwana wa Kosamu, Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu, Elmadamu alikuwa mwana wa Eri, 29 Eri alikuwa mwana wa Yoshua, Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri, Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu, Yorimu alikuwa mwana wa Mathati, Mathati alikuwa mwana wa Lawi, 30 1Lawi alikuwa mwana wa Simeoni, Simeoni alikuwa mwana wa Yuda, Yuda alikuwa mwana wa Yusufu, Yusufu alikuwa mwana wa Yonamu, Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu, Eliakimu alikuwa mwana wa Melea, 31 Melea alikuwa mwana wa Mena, Mena alikuwa mwana wa Matatha, Matatha alikuwa mwana wa Nathani, Nathani alikuwa mwana wa Daudi, 32 Daudi alikuwa mwana wa Yese, Yese alikuwa mwana wa Obedi, Obedi alikuwa mwana wa Boazi, Boazi alikuwa mwana wa Salmoni, Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni, 33 Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu, Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu, Aramu alikuwa mwana wa Hesroni, Hesroni alikuwa mwana wa Peresi, Peresi alikuwa mwana wa Yuda, 34 Yuda alikuwa mwana wa Yakobo, Yakobo alikuwa mwana wa Isaki, Isaki alikuwa mwana wa Abrahamu, Abrahamu alikuwa mwana wa Tera, Tera alikuwa mwana wa Nahori, 35 Nahori alikuwa mwana wa Serugi, Serugi alikuwa mwana wa Ragau, Ragau alikuwa mwana wa Pelegi, Pelegi alikuwa mwana wa Eberi, Eberi alikuwa mwana wa Sala, 36 Sala alikuwa mwana wa Kenani, Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi, Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu, Shemu alikuwa mwana wa Nuhu, Nuhu alikuwa mwana wa Lameki, 37 Lameki alikuwa mwana wa Methusela, Methusela alikuwa mwana wa Henoko, Henoko alikuwa mwana wa Yaredi, Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli, Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani, 38 Kenani alikuwa mwana wa Enoshi, Enoshi alikuwa mwana wa Sethi, Sethi alikuwa mwana wa Adamu,