Akamwona na mama mmoja mjane, maskini sana, akiweka humo sarafu mbili. Akasema, “Nawaambia kweli, huyu mjane ametoa sadaka kubwa zaidi kuliko hao wengine wote. Kwa maana hao wengine wametoa sehemu ndogo tu ya utajiri wao, lakini yeye, ingawa ni maskini, ametoa vyote alivyokuwa navyo.”

Read full chapter