Add parallel Print Page Options

10 Malaika akawaambia, “Msiogope, kwa kuwa nimewaletea habari njema zitakazowafurahisha watu wa Mungu wote. 11 Kwa sababu leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo,[a] Bwana. 12 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: Mtamkuta mtoto mchanga amevingirishiwa nguo na amelala katika hori la kulishia mifugo.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 2:11 Kristo Kwa maana ya kawaida “Kristo”, ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi” linalomaanisha “Mpakwa Mafuta”, ambapo katika Agano la Kale linawakilisha sherehe ya kupakwa mafuta (Kuwekwa Wakfu) mfalme mpya. Pia linamaanisha Mfalme Mteule. Tazama Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno. Pia katika mstari wa 26 na katika kitabu chote hiki.