10 Lakini malaika akawatuliza akisema: “Msiogope! Nawaletea habari njema ya furaha kubwa, na habari hii ni kwa faida ya watu wote! 11 Kwa maana leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa Mwokozi ambaye ndiye Kristo Bwana. 12 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa vinguo na kulazwa horini.”

Read full chapter