Add parallel Print Page Options

Akamjibu, ‘Ananidai mitungi[a] 100 ya mafuta ya zeituni.’ Msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako ya deni, kaa chini, fanya haraka, badilisha iwe mitungi hamsini.’

Kisha akamwambia mwingine, ‘Na wewe kiasi gani unadaiwa?’ Akajibu, ‘Vipimo[b] mia moja vya ngano.’ Akamwambia, ‘Chukua hati yako ya deni, ibadilishe iwe vipimo themanini.’

Baadaye bwana wake akamsifu msimamizi asiye mwaminifu kwa sababu ya kutenda kwa busara. Ndiyo, watu wa ulimwengu huu wana busara katika kufanya biashara kati yao kuliko wana wa Mungu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 16:6 mitungi Kiyunani batous, kutoka kwa Kiebrania bath, sawa na galoni 8 au lita 34.
  2. 16:7 Vipimo Kiyunani korous, kutoka kwa Kiebrania cor, kipimo sawa kama galoni 89 au lita 390.