Add parallel Print Page Options

Yesu Asema Petro Atamkana

(Mt 26:31-35; Mk 14:27-31; Lk 22:31-34)

36 Simoni Petro akamwuliza Yesu, “Bwana, unaenda wapi?”

Yesu akajibu, “Kule niendako hamwezi kunifuata sasa. Lakini mtanifuata baadaye.”

37 Petro akauliza, “Bwana, kwa nini nisikufuate sasa? Mimi niko radhi kufa kwa ajili yako!”

38 Yesu akajibu, “Je, ni kweli utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Hakika nakwambia, kabla jogoo hajawika, utasema mara tatu kwamba hunijui mimi.”

Yesu Awafariji Wafuasi Wake

14 Yesu akasema, “Msisumbuke. Mwaminini Mungu, na mniamini na mimi.