Neno Alifanyika Mwili

Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba.

Read full chapter

Yesu ni Neno la Mungu la Milele

Mwanzoni Kabla ulimwengu haujaumbwa
    alikuwepo Neno.[a]
Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu,
    na Neno alikuwa Mungu.
Alikuwepo pamoja na Mungu
    toka mwanzo.
Kila kitu kilifanyika kupitia kwake.
    Hakuna chochote katika uumbaji wa Mungu
    kilichofanyika bila yeye.

Read full chapter

Notas al pie

  1. 1:1 Neno Kwa Kiyunani neno hili ni logos, lenye maana mawasiliano ya aina yoyote. Linaweza kutafsiriwa “ujumbe”. Hapa lina maana ya Kristo; njia ambayo Mungu alitumia kuueleza ulimwengu kuhusu yeye. Pia katika mstari wa 10,14 na 16.