Matendo Ya Mitume 20:7-12
Neno: Bibilia Takatifu
Paulo Akutana Na Waamini Wa Troa
7 Jioni siku ya kwanza ya Juma tulikuwa tumekutana pamoja kwa chakula na Paulo akaongea nao akiwa na mpango wa kuondoka kesho yake; akaendelea na mazungumzo mpaka usiku wa manane. 8 Chumba cha ghorofani walipokuwa wakikutania kilikuwa na taa nyingi 9 na kijana mmoja jina lake Eutiko alikuwa amekaa dirishani. Paulo alivyoendelea kuongea kijana huyu alizidi kusinzia. Hatimaye alishikwa na usingizi kabisa, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu, akadhaniwa kuwa amekufa. 10 Lakini Paulo alishuka chini akainama, akamkumbatia yule kijana akasema, “Msiwe na hofu, yun gali hai.” 11 Paulo akarudi ghorofani na alipokwisha kula, akaongea nao tena mpaka alfajiri ndipo akaondoka. 12 Yule kijana alichukuliwa nyumbani akiwa hai na wote waliokuwepo walifarijika.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica