Kuja Kwa Bwana Na Kudhihirishwa Kwa Mwovu

Basi, kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu mbele zake, tunawasihi, ndugu wapendwa, msifadhaike au kuwa na wasiwasi kutokana na utabiri fulani, au taarifa au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, kusema eti kwamba siku ya Bwana imekwisha kuja. Mtu asiwadanganye kwa namna yo yote maana siku hiyo haitakuja kabla ya uasi kutokea kwanza na yule mwasi adhi hirishwe, yule ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa. Yeye anapinga kila ambacho watu hukiita mungu au cho chote kinachoabu diwa; naye hujiweka hata katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.

Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambieni mambo haya? Na mnajua kinachomzuia sasa, ili adhihirishwe wakati ufaao. Maana ile nguvu ya siri ya uasi imekwisha anza kufanya kazi; lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. Hapo ndipo yule mwovu ataonekana, na Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa ufahari wa kuja kwake. Kuja kwa yule mwovu kutafuata kazi ya shetani ambayo itaonyeshwa katika aina zote za ishara bandia na maajabu ya uongo; 10 na katika kila aina ya uovu unaotumiwa kuwadanganya wale wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 11 Ndio maana Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu ili waendelee kuu amini uongo; 12 na ili wote wasioamini kweli bali hufurahia uovu, wahukumiwe.

Simameni Imara

13 Lakini tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, maana Mungu aliwachagueni tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho na kwa kuiamini kweli. 14 Mungu amewaitieni jambo hili kwa njia ya mahubiri yetu ya Habari Njema, ili muweze kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 15 Kwa hiyo ndugu wapendwa, simameni imara na mshike sana yale mafundisho tuliyowapeni katika mahubiri yetu na kwa barua zetu.

16 Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, ali yetupenda akatupatia faraja ya milele na tumaini jema kwa neema, 17 na awafariji mioyoni mwenu na kuwaimarisheni katika kila jambo jema mnalosema au kutenda.