Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wathes alonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. Tuna watakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.

Sala Na Shukrani

Hatuna budi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu wapendwa; na ndivyo inavyostahili kwa sababu imani yenu inaongezeka zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu kwa mwen zake unazidi kuongezeka. Ndio maana sisi tunajivuna kwa ajili yenu miongoni mwa makanisa ya Mungu. Tunajivuna juu ya uvumilivu wenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazopata.

Haya yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtastahili kupata Ufalme wa Mungu ambao mnateswa kwa ajili yake. Mungu ni wa haki: atawalipa kwa mateso wale wanaowatesa ninyi na kuwapeni ninyi mnaoteseka nafuu pamoja na sisi pia. Haya yatatokea wakati Bwana Yesu atakapodhi hirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake, 10 siku ile atakapokuja kutukuzwa kwa ajili ya watakatifu wake na kustaajabiwa na watu wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa mion goni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.

11 Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnastahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu. 12 Tunaomba hivi ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwa ajili yenu nanyi mtukuzwe kwa ajili yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.