Add parallel Print Page Options

Wataadhibiwa na maangamizi yasio na mwisho. Hawataruhusiwa kuwa na Bwana lakini watatengwa mbali na nguvu zake za utukufu. 10 Hii itatokea siku ambapo Bwana Yesu atakuja na kupokea heshima miongoni mwa watu wake watakatifu. Na wote wanaomwamini watamstaajabu. Na hii inawajumuisha ninyi kwa sababu mliamini yale tuliyowaambia.

11 Hii ndiyo sababu daima tunawaombea. Tunamwomba Mungu wetu awasaidie kuishi katika njia njema aliyoitaka alipowachagua. Wema mlionao unawafanya mtake kufanya mema. Na imani mliyonayo inafanya mfanye kazi. Tunaomba kwamba kupitia nguvu zake Mungu atayakamilisha yote mema mliyokusudia kufanya pamoja na kazi zote zinazotokana na imani yenu.

Read full chapter