Font Size
2 Wathesalonike 1:9-11
Neno: Bibilia Takatifu
2 Wathesalonike 1:9-11
Neno: Bibilia Takatifu
9 Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake, 10 siku ile atakapokuja kutukuzwa kwa ajili ya watakatifu wake na kustaajabiwa na watu wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa mion goni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
11 Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnastahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica