Sala Na Shukrani

Hatuna budi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu wapendwa; na ndivyo inavyostahili kwa sababu imani yenu inaongezeka zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu kwa mwen zake unazidi kuongezeka. Ndio maana sisi tunajivuna kwa ajili yenu miongoni mwa makanisa ya Mungu. Tunajivuna juu ya uvumilivu wenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazopata.

Haya yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtastahili kupata Ufalme wa Mungu ambao mnateswa kwa ajili yake.

Read full chapter