Kwa kuwa tumepewa ahadi hizi wapendwa, basi tujitakase kutokana na kila aina ya uchafu wa mwili na roho, na tufanye bidii kufikia ukamilifu kwa kuwa tunamcha Mungu.

Furaha Ya Paulo

Tupokeeni kwa moyo mweupe. Hatujamkosea mtu ye yote, hatu jampotosha mtu ye yote, wala hatujamdhulumu mtu ye yote. Sisemi haya ili kuwahukumu; kwa kuwa, kama nilivyosema mwanzo, tunawath amini kiasi ambacho mpo mioyoni mwetu wakati wote, ikiwa ni kufa pamoja au kuishi pamoja. Ninayo imani kubwa kwenu; ninawaonea fahari kubwa. Nimefarijika sana. Pamoja na taabu zetu zote, furaha yangu haina mfano.

Kwa maana hata tulipofika Makedonia, miili yetu haikuwa na amani. Tulitaabishwa kila upande, kwa nje kulikuwa na upinzani na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu. Bali Mungu, ambaye hufariji wenye huzuni, alitufariji kwa kumleta Tito; na si kwa kuwa Tito alifika tu, bali pia kwa kuwa ninyi mlimfariji. Alitueleza juu ya upendo wenu, huzuni yenu na jinsi mlivyonihurumia, kwa hiyo furaha yangu iliongezeka sana.

Hata kama barua yangu iliwasikitisha, sasa sijuti kwamba niliiandika ingawa nilikuwa nimejuta. Naona barua yangu iliwahu zunisha, lakini kwa muda mfupi. Lakini sasa ninafurahi, si kwa kuwa mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunika kama Mungu anavyopenda watu wahuzunike na hivyo hatukuwadhuru kwa njia yo yote. 10 Kwa maana huzuni ikitumiwa na Mungu huwafanya watu watubu dhambi zao wapate kuokolewa; nao wanakuwa hawana majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha kifo. 11 Tazameni faida mlizopata kutokana na huzuni hii: bidii mliyo nayo; juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu, na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmethibitisha kuwa hamna hatia katika jambo hilo. 12 Kwa hiyo ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe muone, mbele za Mungu, jinsi mnavyotupenda kwa moyo wote. 13 Kwa hiyo tumefarijika. Pamoja na faraja tuliyopata, tumefu rahi zaidi kwa kuona jinsi Tito alivyofurahi kwa kuwa mlimwondo lea wasi wasi aliokuwa nao. 14 Nilikuwa nimejisifu kwake juu yenu nanyi hamkuniaibisha. Kama jinsi yale niliyowaambia yalivy okuwa ya kweli, hali kadhalika kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumeonekana kuwa kweli pia. 15 Upendo wake kwenu unaongezeka sana anapokumbuka jinsi mlivyokuwa watii na jinsi mlivyompokea kwa hofu na kutetemeka. 16 Nafurahi kwa sababu nina imani nanyi kabisa.