15 Kuna kuelewana gani kati ya Kristo na shetani? Mwamini ana uhusiano gani na asiyeamini? 16 Kuna uelewano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema, “Nitaishi ndani yao na kutembea kati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkajitenge nao, asema Bwana. Msiguse cho chote kisicho safi; ndipo nitawakaribisha kwangu.

Read full chapter