Wahudumu Wa Agano Jipya

Je mnadhani tunaanza kujisifu tena? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine wafanyavyo? Ninyi wenyewe ni barua yetu ya utambulisho iliyoan dikwa katika mioyo yenu, ijulikane na kusomwa na kila mtu. Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, matokeo ya kazi yetu. Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai.

Hili ndilo tumaini tulilo nalo kwa Mungu ndani ya Kristo. Haina maana kwamba sisi tunaweza wenyewe kupima cho chote tuna chofanya, lakini uwezo wetu unatoka kwa Mungu. Ni yeye ali yetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya, ambalo limefanywa, si kwa maandishi, bali kwa Roho. Kwa maana maandishi huleta kifo, lakini Roho huleta Uzima.

Utukufu Wa Agano Jipya

Sasa ikiwa huduma iliyoleta kifo, ambayo iliandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata ikawa Waisraeli wal ishindwa kutazama uso wa Musa kwa sababu ya kung’aa kwake, ingawa ulikuwa ukififia, je? Huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? Ikiwa huduma inayowahukumu watu ina utukufu, huduma inayoleta haki si itakuwa na utukufu zaidi? 10 Hakika kwa hali hii, kilichokuwa na utukufu hapo mwanzo, sasa hakina utukufu tena kikilinganishwa na utukufu uliopo. 11 Na kama kilichokuwa kina fifia kilikuja kwa utukufu, utukufu wa kile kinachodumu ni zaidi sana!

12 Kwa hiyo kwa kuwa tunatumaini hili, tuna ujasiri. 13 Sisi si kama Musa, ambaye alifunika uso wake kwa kitambaa ili Waisraeli wasione ule mng’ao ulivyokuwa ukififia na kutoweka. 14 Lakini akili zao zilipumbaa, kwa maana mpaka leo akili zao zinafunikwa na kitambaa wakati agano jipya linaposomwa. Hicho kitambaa hakijaondolewa kwa maana ni Kristo peke yake anayeweza kukiondoa. 15 Hata leo, sheria ya Musa inaposomwa, bado kitambaa kinafunika akili zao. 16 Lakini wakati wo wote mtu anapomgeukia Bwana, “kitambaa kinaondolewa.” 17 Basi, Bwana ni Roho, na mahali alipo Roho wa Bwana pana uhuru. 18 Na sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa tunaonyesha, kama kwenye kioo, utukufu wa Bwana. Nasi tunabadilishwa tufanane naye, kutoka utukufu hadi utukufu wa juu zaidi, ambao unatoka kwa Bwana ambaye ni Roho.