Kwa sababu hiyo, niliamua kwamba sitafanya safari nyingine kuja kuwahuzunisha. Kwa kuwa kama nawahuzunisha, ni nani ali yebaki kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? Ndio sababu nikawaandikia ili nitakapokuja nisihuzunishwe na watu ambao wangenifanya nifurahi. Nilikuwa na uhakika kwenu kwamba furaha yangu ingekuwa furaha yenu nyote. Kwa maana nili waandikia katika dhiki na kutaabika moyoni na kwa machozi mengi. Shabaha yangu haikuwa kuwahuzunisha bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.

Msamaha Kwa Mwenye Dhambi

Basi ikiwa mtu ye yote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama alivyowahuzunisha ninyi nyote; sipendi kuweka uzito zaidi kwa upande wenu. Basi adhabu aliyop ewa na wengi inamtosha. Na sasa mnapaswa kumsamehe na kumfariji ili asikate tamaa kabisa kutokana na huzuni kubwa mno aliyo nayo. Kwa hiyo nawasihi mumhakikishie tena kwamba mnampenda. Nili waandikia kuwajaribu ili nione kama mtakuwa watii kwa kila kitu. 10 Mtu ye yote mnayemsamehe na mimi namsamehe. Cho chote nili chosamehe, kama kulikuwa na cha kusamehe, nimesamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo 11 ili shetani asije akatushinda. Kwa maana tunajua mipango yake.

12 Nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo, nilikuta Bwana ameshafungua mlango. 13 Lakini sikuweza kutulia kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Kwa hiyo nikaagana nao nikaenda Makedonia.

Ushindi Ndani Ya Kristo

14 Lakini Mungu ashukuriwe, ambaye hutuongoza katika ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye hututumia sisi kueneza maarifa ya kumjua yeye kila mahali kama harufu nzuri. 15 Kwa Mungu sisi ni kama harufu nzuri ya manukato ya Kristo ambayo inatapakaa mion goni mwa wale wanaookolewa na wale wanaopotea. 16 Kwa wale wanaopotea sisi ni kama harufu ya kifo, lakini kwa wale wanaooko lewa sisi ni harufu iletayo uzima. Ni nani basi awezaye kufanya kazi hiyo? 17 Sisi si kama watu wengine ambao wanauza neno la Mungu wajipatie faida. Lakini kama watu wenye moyo safi, tuliot euliwa na Mungu mbele yake mwenyewe, sisi tunazungumza tukiwa ndani ya Kristo.