Add parallel Print Page Options

15 Maisha yetu ni sadaka ya harufu nzuri ya manukato ya Kristo inayotolewa kwa Mungu. Harufu nzuri ya sadaka hii huwaendea wale wanaokolewa na kwa wale wanaopotea. 16 Kwao wanaopotea, marashi haya yananukia kama mauti, na huwaletea kifo. Ila kwao wanaookolewa, ina harufu nzuri ya uzima, na inawaletea afya ya uzima. Kwa hiyo ni nani aliye bora kuifanya kazi hii? 17 Kwa hakika sio wale wanaozunguka wakiuuza ujumbe wa Mungu ili kupata faida! Lakini sisi hatufanyi hivyo. Kwa msaada wa Kristo tunaisema kweli ya Mungu kwa uaminifu, tukifahamu kuwa tunazungumza kwa ajili yake na mbele zake.

Read full chapter