2 Wakorintho 2:14-3:6
Neno: Bibilia Takatifu
Ushindi Ndani Ya Kristo
14 Lakini Mungu ashukuriwe, ambaye hutuongoza katika ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye hututumia sisi kueneza maarifa ya kumjua yeye kila mahali kama harufu nzuri. 15 Kwa Mungu sisi ni kama harufu nzuri ya manukato ya Kristo ambayo inatapakaa mion goni mwa wale wanaookolewa na wale wanaopotea. 16 Kwa wale wanaopotea sisi ni kama harufu ya kifo, lakini kwa wale wanaooko lewa sisi ni harufu iletayo uzima. Ni nani basi awezaye kufanya kazi hiyo? 17 Sisi si kama watu wengine ambao wanauza neno la Mungu wajipatie faida. Lakini kama watu wenye moyo safi, tuliot euliwa na Mungu mbele yake mwenyewe, sisi tunazungumza tukiwa ndani ya Kristo.
Wahudumu Wa Agano Jipya
3 Je mnadhani tunaanza kujisifu tena? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine wafanyavyo? 2 Ninyi wenyewe ni barua yetu ya utambulisho iliyoan dikwa katika mioyo yenu, ijulikane na kusomwa na kila mtu. 3 Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, matokeo ya kazi yetu. Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai.
4 Hili ndilo tumaini tulilo nalo kwa Mungu ndani ya Kristo. 5 Haina maana kwamba sisi tunaweza wenyewe kupima cho chote tuna chofanya, lakini uwezo wetu unatoka kwa Mungu. 6 Ni yeye ali yetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya, ambalo limefanywa, si kwa maandishi, bali kwa Roho. Kwa maana maandishi huleta kifo, lakini Roho huleta Uzima.
Marko 10:1-16
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Afundisha Kuhusu Talaka
10 Yesu akaondoka mahali pale akavuka mto wa Yordani, akaenda sehemu ya Yudea. Umati wa watu ukamfuata tena na kama kawaida yake akawafundisha.
2 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakitaka kumtega, wakamwul iza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake?”
3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuruje?” 4 Wakamjibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”
5 Yesu akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke. 7 Na kwa sababu hii mume atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ 8 Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. 9 Basi, alichokiun ganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
10 Baadaye waliporudi nyumbani , wanafunzi wa Yesu walimwul iza kuhusu jambo hili.
11 Akawajibu, “Mtu ye yote anayempa mkewe talaka na kuoa mke mwingine, anazini kwa yule mke aliyempa talaka. 12 Na mwa namke anayempa mumewe talaka na kuolewa na mume mwingine, anazini pia.”
Yesu Anawabariki Watoto Wadogo
13 Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14 Yesu alipoona yaliyokuwa yakitokea alichukizwa, akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu kama hawa! 15 Ninawahakikishieni kwamba, mtu ye yote ambaye hataukubali Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” 16 Akawakumbatia wale watoto wadogo, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica