Maagizo Ya Mwisho

Ninakuamuru mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu ambaye atawahukumu walio hai na wafu; na kwa kuja kwake na ufalme wake: hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti. Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo. Bali wewe uwe imara, katika mambo yote, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

Maana mimi sasa ni tayari kutolewa kama sadaka, saa ya kuondoka kwangu imefika. Nimepigana ile vita njema, nimemaliza shindano, nimeitunza imani. Na sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanituza Siku ile; wala si mimi tu, bali na wote ambao wamengojea kwa hamu kuja kwake.

Maombi Ya Binafsi

Jitahidi kuja kuniona upesi 10 kwa sababu Dema, kwa kuu penda ulimwengu huu wa sasa, ameniacha akaenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia.

11 Ni Luka peke yake ambaye yupo hapa pamoja nami. Mchukue Marko uje pamoja naye kwa sababu ananisaidia katika huduma yangu. 12 Nimemtuma Tikiko Efeso. 13 Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu, hasa vile vya ngozi.

14 Aleksanda mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Mungu atamlipa kwa yale aliyonitendea. 15 Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu alipinga vikali ujumbe wetu.

16 Nilipojitetea mara ya kwanza hakuna hata mmoja aliyekuwa upande wangu, kila mmoja alinikimbia. Naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama nami akanitia nguvu kutangaza Habari Njema kwa ukamilifu ili watu wote wa mataifa wapate kusikia. Na niliokolewa kutoka katika kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa katika kila uovu na kunihifadhi mpaka niu fikie ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe Yeye milele na milele.

Salamu Za Mwisho

19 Nisalimie Prisila na Akila na wote waliomo nyumbani kwa Onesiforo. 20 Erasto alibaki Korintho. Trofimo nilimwacha akiwa mgonjwa huko Mileto.

21 Jitahidi kufika huku kabla ya majira ya baridi kali. Sal amu zako kutoka kwa Eubulo, Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.