16 Jiepushe na maneno ya kipuuzi, yasiyo ya kimungu, kwa maana hayo huwavuta watu mbali na Mungu zaidi na zaidi. 17 Mafundisho yao yataendelea kuenea kama donda ndugu. Kati yao wamo Himenayo na Fileto 18 ambao wametanga tanga na kuiacha kweli wakisema kwamba ufufuo umekwishapita. Wanapotosha imani ya baadhi ya watu.

Read full chapter