Walimu Wa Uongo

Lakini pia walikuwepo manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyotokea walimu wa uongo kati yenu. Kwa siri, watain giza mafundisho ya upotovu hata kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watajiletea maangamizi ya haraka. Na wengi wata fuata tamaa zao potovu, na kwa ajili ya matendo yao njia ya kweli itadharauliwa. Nao katika tamaa yao watajaribu kuwanunua kwa kuwaambia hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu yao imekuwa tayari tangu zamani, wala mwangamizi wao hajalala usingizi.

Maana kama Mungu hakuwahurumia malaika walipotenda dhambi bali aliwatupa kuzimu, katika vifungo vya giza wakae huko mpaka siku ya hukumu; kama hakuuhurumia ulimwengu wa kale alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiomcha Mungu, akamlinda Noe mjumbe wa haki, pamoja na watu saba wengine; kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza ikawa majivu, akaifanya kuwa mfano kwa wote ambao hawatamcha Mungu; na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki ambaye alihuzunishwa na maisha ya uchafu ya watu wahalifu - kwa sababu yale maasi aliyoona na kusikia huyo mtu wa Mungu alipoishi kati yao yalimhuzunisha usiku na mchana - basi ikiwa ni hivyo, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wa Mungu kutoka katika majaribu na kuwaweka waasi katika hali ya adhabu mpaka siku ya hukumu. 10 Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa chafu za mwili na kudharau mamlaka. Watu hawa ni shupavu na katika kiburi chao, hawaogopi kuwatu kana viumbe vitukufu wa mbinguni;

11 ingawa hata malaika, ambao wana nguvu na uwezo zaidi, hawawashtaki au kuwatukana viumbe hao mbele za Bwana. 12 Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiy oyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawal iwa na hisia za mwili, ambao wamezaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa, na kama wanyama, wao pia wataangamizwa.

13 Watalipizwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Furaha yao ni kufanya karamu za ufisadi mchana, wazi wazi. Wao huleta aibu na fedheha wanaposhiriki katika karamu zenu kwa kuwa wakati wote huo, wanajifurahisha katika upotevu wao. 14 Macho yao yamejaa uzinzi, nao hutenda dhambi bila kikomo. Huwahadaa watu dhaifu. Mioyo yao imezoea kutamani. Hawa ni wana wa laana! 15 Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa kupata fedha kwa kufa nya maovu. 16 Balaamu alikaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinena kwa sauti ya binadamu akamzuia huyo nabii asiendelee na kichaa chake.

17 Watu hawa ni kama chemchemi zilizokauka na ukungu upeper ushwao na tufani, na lile giza jeusi limewekwa tayari kwa ajili yao. 18 Wao hutamka maneno matupu ya majivuno na kutumia tamaa mbaya za mwili kuwanasa tena wale ambao ndio kwanza wameepukana na watu wanaoishi maisha ya uovu. 19 Huwaahidi hao waliowanasa kuwa watakuwa huru kabisa, lakini wao wenyewe ni watumwa wa upo tovu. Kwa maana mtu huwa mtumwa wa kitu kile kinachomshinda nguvu. 20 Kwa maana wale waliokwisha kuponyoka kutoka katika uchafu wa dunia hii kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo , kisha wakanaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. 21 Ingekuwa heri kwao kama hawa kuijua kamwe njia ya haki, kuliko kuifahamu kisha wakaiacha ile amri takatifu waliyopewa. 22 Kama methali moja isemavyo, “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine, “Nguruwe huoshwa na kurudi kugaa-gaa matopeni.”