2 Petro 1:12-21
Neno: Bibilia Takatifu
Unabii Wa Maandiko
12 Kwa hiyo ninakusudia kuwakumbusha hayo siku zote, ingawa mnayafahamu na mmekuwa imara katika kweli mliyo nayo. 13 Nadhani ni vema niwahimize kwa kuwakumbusha mambo haya, wakati wote nina poishi katika mwili huu. 14 Kwa maana najua kwamba karibu nitauweka kando mwili wangu, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyon ionyesha wazi. 15 Na nitahakikisha kwamba baada ya kuondoka kwangu mtaendelea kukumbuka mambo haya kila wakati.
16 Tulipowafundisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulish uhudia kwa macho yetu utukufu wake. 17 Maana alipopewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, na sauti ikamjia katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye’ 18 tuliisikia sauti hii iliyotoka mbinguni, maana tulikuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.
19 Kwa hiyo tuna uhakika zaidi juu ya ujumbe wa manabii. Hivyo itakuwa vema mkizingatia ujumbe huo, kama vile watu wanavy oitegemea taa ing’aayo mahali penye giza, mpaka Siku ile itakapo fika na nyota ya asubuhi itakapoangaza mioyoni mwenu. 20 Kwanza kabisa ni lazima muelewe kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliotokana na tafsiri ya nabii mwenyewe. 21 Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Read full chapter

Luka 22:54-69
Neno: Bibilia Takatifu
Petro Amkana Yesu
54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57 Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe pia ni mmoja wao.” Petro akajibu, “Bwana, mimi si mmoja wao!” 59 Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akasisitiza, “Kwa hakika huyu mtu alikuwa na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60 Petro akajibu, “Mimi sijui unalosema!” Na wakati huo huo, akiwa bado anazun gumza, jogoo akawika. 61 Yesu akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62 Akaenda nje, akalia kwa uchungu . Yesu Achekwa Na Kupigwa
63 Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64 Wakamfunga kitambaa usoni kisha wakasema, “Hebu nabii tuambie! Ni nani amekupiga?” 65 Wakamwambia maneno mengi ya kumtukana. Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza
66 Kulipokucha, Baraza la wazee wa Wayahudi, makuhani wakuu na walimu wa sheria wakakutana. Yesu akaletwa mbele yao. 67 Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawa jibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini, 68 na nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 Lakini hivi karibuni, mimi Mwana wa Adamu nita kaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.”

Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica