1 Yohana 5:14-20
Neno: Bibilia Takatifu
14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia. 15 Na tukijua kwamba anatusikia kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale tuliyomwomba.
Umuhimu Wa Kuonyana
16 Mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyompeleka kwe nye kifo, amwombee kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Ninasema kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi ambayo humpeleka mtu kwenye kifo. Sisemi kwamba ana paswa kuomba kuhusu hiyo. 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi na kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.
18 Tunafahamu kuwa kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda na yule mwovu hawezi kumgusa. 19 Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na kwamba ulim wengu wote unatawaliwa na yule mwovu. 20 Tunajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupa ufahamu ili tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica