Kujihadhari Na Maadui Wa Kristo

Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani. Na hivi ndivyo mtakavyomtambua Roho wa Mungu: kila roho inayokiri kuwa Yesu Kristo alikuja kama mwana damu, hiyo inatoka kwa Mungu. Lakini roho yo yote ambayo haim kiri Kristo, si ya Mungu. Hii ndio roho ya mpinga-Kristo, ambayo mmekwisha kusikia kwamba inakuja, na sasa tayari iko duniani.

Lakini ninyi watoto wapendwa, ni wa Mungu, nanyi mmekwisha kuwashinda; kwa maana yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yule aliyeko duniani. Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanayoyasema ni ya ulimwengu na watu wa dunia huwasikiliza. Sisi ni wa Mungu. Anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiye wa Mungu hatusikilizi. Na hivi ndivyo tunaweza kutambua kati ya Roho wa kweli na roho wa uongo.

Mungu Ni Upendo

Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu. 11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona. 21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.