1 Yohana 4:7-5:20
Neno: Bibilia Takatifu
Mungu Ni Upendo
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu. 11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona. 21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.
Imani Ndani Ya Kristo
5 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo, ni mtoto wa Mungu; na kila ampendaye mzazi wa mtoto, humpenda pia na mtoto wa mzazi huyo. 2 Na hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: tukimpenda Mungu na kuzitii amri zake. 3 Kwa maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na amri zake hazitule mei. 4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu ameushinda ulimwengu. Nasi tumeushinda ulimwengu kwa imani yetu. 5 Ni nani basi aushin daye ulimwengu isipokuwa yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
Mashahidi Wa Yesu Kristo
6 Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji na damu; si kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Roho mwenyewe ndiye anayemshu hudia kwa maana Roho ni kweli. 7 Wapo mashahidi watatu: 8 Roho, maji na damu; na hawa watatu wanakubaliana. 9 Kama tunakubali ushahidi wa wanadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; kwa sababu huu ni ushahidi wa Mungu ambao ameutoa kumhusu Mwanae. 10 Mtu anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake. Mtu asiyemwamini Mungu, amemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda alioutoa Mungu kuhusu Mwanae. 11 Na ushuhuda wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo kwa Mwanae. 12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.
Uzima Wa Milele
13 Ninawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu kusudi mjue kuwa mnao uzima wa milele. 14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia. 15 Na tukijua kwamba anatusikia kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale tuliyomwomba.
Umuhimu Wa Kuonyana
16 Mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyompeleka kwe nye kifo, amwombee kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Ninasema kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi ambayo humpeleka mtu kwenye kifo. Sisemi kwamba ana paswa kuomba kuhusu hiyo. 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi na kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.
18 Tunafahamu kuwa kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda na yule mwovu hawezi kumgusa. 19 Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na kwamba ulim wengu wote unatawaliwa na yule mwovu. 20 Tunajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupa ufahamu ili tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
2 Yohana
Neno: Bibilia Takatifu
1 Kutoka kwa Mzee. Kwa mama mteule pamoja na watoto wake niwapendao katika kweli. Wala si mimi tu niwapendaye bali wote wanaoifahamu kweli; 2 kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itakuwa nasi hadi milele.
3 Neema, huruma, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wake zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
Kweli Na Upendo
4 Nimefurahi sana kuona kwamba baadhi ya watoto wako wanadumu katika kweli, kama Baba alivyotuamuru. 5 Na sasa, mama mpendwa, sikuandikii amri mpya, bali ile ile ambayo tumekuwa nayo kutoka mwanzo: kwamba tupendane. 6 Na upendo ni huu: kwamba tuishi kwa kuzifuata amri za Mungu. Na kama mlivyosikia tangu mwanzo, amri yake ni kwamba muishi maisha ya upendo.
7 Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, watu wasiokiri ya kwamba Kristo alikuja kama mwanadamu. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na mpinga-Kristo. 8 Jihadharini msije mkapoteza yale mliyoyafanyia kazi, bali mpewe thawabu kamili.
9 Mtu ye yote anayevuka mpaka wa mafundisho ya Kristo, na kuyaacha, huyo hana Mungu. Na mtu anayedumu katika mafundisho ya Kristo, huyo anaye Baba na Mwana pia. 10 Mtu ye yote akija kwenu bila kuwaletea mafundisho haya, msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu. 11 Kwa maana mtu anayemsalimu anashiriki kazi zake za uovu.
12 Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sipendi kutumia kara tasi na wino. Badala yake ninatarajia kuwatembelea na kuongea nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu ikamilike.
3 Yohana
Neno: Bibilia Takatifu
1 Kutoka Kwa Mzee. Kwa mpendwa wangu Gayo, nimpendaye katika kweli. 2 Mpendwa, ninakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kwamba uwe na afya njema ya mwili; kwa maana najua roho yako ni salama. 3 Nilifurahi sana walipokuja ndugu kadhaa wakashuhudia jinsi ulivyo mwaminifu katika kweli na jinsi unavyoendelea kuishi katika kweli. 4 Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusi kia kwamba watoto wangu wanafuata kweli.
Uaminifu Wa Gayo
5 Mpendwa, wewe umekuwa mwaminifu kwa yote unayowatendea hao ndugu, ingawaje wao ni wageni kwako. 6 Wamelishuhudia kanisa kuhusu upendo wako. Tafadhali wasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu. 7 Kwa maana wanasafiri kwa ajili ya Bwana na wamekataa kupokea cho chote kutoka kwa watu wasiomjua Mungu . 8 Kwa hiyo tunawajibu wa kuwasaidia watu wa namna hiyo ili tuwe watenda kazi pamoja nao kwa ajili ya kweli.
Diotrefe Na Demetrio
9 Niliandika barua kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe apendaye kujiweka mbele kama kiongozi wao, hatambui mamlaka yangu. 10 Kwa hiyo nitakapokuja nitaeleza mambo anayofanya; na kuhusu maneno maovu anayosema juu yangu. Wala hatosheki na hayo bali anakataa kuwakaribisha ndugu. Pia anawazuia wale ambao wanataka kuwakarib isha na anawafukuza kutoka katika kanisa. 11 Mpendwa, usiige ubaya bali iga wema. Atendaye mema ni wa Mungu. Atendaye uovu hajapata kumwona Mungu. 12 Demetrio anashuhudiwa wema na kila mtu na hata kweli yenyewe inamshuhudia. Mimi pia ninamshuhudia wema, na wewe unajua kwamba ushuhuda wangu ni wa kweli.
Salamu Za Mwisho
13 Ninayo mengi ya kukuandikia, lakini afadhali nisitumie kalamu na wino. 14 Natarajia kukuona karibuni na tutaongea uso kwa uso.
Copyright © 1989 by Biblica