1 Yohana 4:7-21
Neno: Bibilia Takatifu
Mungu Ni Upendo
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu. 11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona. 21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.
Read full chapter
Yohana 11:30-44
Neno: Bibilia Takatifu
30 Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini. Alikuwa bado yuko pale Martha alipokutana naye. 31 Wale Wayahudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walipoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwa hiyo wakamfuata. 32 Mariamu alipomwona Yesu aliinama chini kwa heshima akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu han galikufa.” 33 Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni; 34 akau liza, “Mmemzika wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.” 35 Yesu akalia. 36 Wale Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!” 37 Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwa nini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”
Yesu Amfufua Lazaro
38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe. 39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.” 40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. 42 Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.” 43 Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!” 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!”
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica