Bwana Atakuja Ghafla

Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. Wakati watu bado wanasema, “Kuna amani na usalama’

Bali ninyi, ndugu wapendwa, hamko gizani kuhusu mambo haya hata siku ile iwashtue kama mwizi. Ninyi nyote ni wana wa nuru, wana wa mchana. Sisi sio watu wa giza au wa usiku. Kwa hiyo basi, tusiwe kama baadhi ya watu wengine, waliolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. Maana wale wanaolala hulala usiku, na wale wanaolewa hulewa usiku. Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukivaa imani na upendo kama kinga ya kifuani na kuvaa tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. Maana Mungu hakutuchagua ili tupate ghadhabu yake bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 10 Yeye alitufia ili kama tuko hai au hata kama tumekufa, tuishi pamoja naye. 11 Kwa hiyo farijianeni na kujengana kama mnavyofanya sasa.

Maagizo Ya Mwisho Na Salamu

12 Sasa tunawaomba, ndugu wapendwa, muwaheshimu wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu; ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. 13 Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao. Ishini kwa amani kati yenu. 14 Na tunawasihi, ndugu wapendwa, muwaonye wale walio wavivu, watieni moyo walio waoga, wasaidieni walio dhaifu na muwe na subira na kila mtu. 15 Hakikisheni kuwa mtu hamlipi mwenzake ovu kwa ovu bali daima jitahidini kutendeana wema ninyi kwa ninyi na watu wengine wote.

16 Furahini wakati wote, 17 ombeni pasipo kukoma, 18 shu kuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu. 19 Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 20 msidharau unabii. 21 Pimeni kila kitu. Yash ikeni kwa makini yaliyo mema. 22 Epukeni uovu wa kila namna.

23 Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase kabisa. Roho zenu, nafsi zenu na miili yenu na ihifadhiwe bila kuwa na lawama kwa wakati atakapokuja Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye aliyew aita ni mwaminifu naye atafanya haya.

25 Ndugu wapendwa, tuombeeni. 26 Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. 27 Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii.