Huduma Ya Paulo Huko Thesalonike

Wapendwa, ninyi wenyewe mnajua kwamba tulipokuja kwenu haikuwa bure. Kama mjuavyo tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu, tulikuwa na uja siri wa kuwaambia Habari Njema ya Mungu pamoja na kwamba uliku wapo upinzani mkali. Ujumbe wetu kwenu hautokani na kutokujua au nia mbaya au udanganyifu. Kinyume chake, tunahubiri kama watu tuliopata kibali cha Mungu tukakabidhiwa Habari Njema. Nia yetu si kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu anayejua mawazo ya mioyo yetu. Mnafahamu kuwa hatukutumia maneno matamu ya kujipendekeza kwenu, wala hatukutumia hila kuficha tamaa ya kujipatia fedha, kwa maana Mungu ni shahidi yetu. Hatukutafuta kupata sifa kutoka kwa mwanadamu ye yote, kwenu au kwa mtu mwin gine.

Kama mitume wa Kristo tungaliweza kudai heshima kutoka kwenu, lakini tulikuwa wapole kwenu kama mama anayetunza watoto wake wadogo. Tuliwapenda sana, kiasi kwamba tulifurahi kushiri kiana nanyi, si Habari Njema ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa maana tuliwathamini mno. Ndugu zetu, bila shaka mnakumbuka juhudi yetu na kutaabika kwetu. Tulifanya kazi usiku na mchana kusudi tusiwe mzigo kwa mtu ye yote wakati tunawahubiria Habari Njema ya Mungu. 10 Ninyi ni mashahidi na Mungu pia ni shahidi yetu kwamba tulikuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama kati yenu mlioamini. 11 Maana mnajua jinsi tulivyowatendea kama baba awa tendeavyo watoto wake: 12 tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwa himiza muishi maisha yampendezayo Mungu, ambaye anawaita mshiriki ufalme wake na utukufu.

13 Nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma pia kwa sababu mlipo lipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu. Bali mlilipokea kama lilivyo hasa, yaani, neno la Mungu, ambalo linafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. 14 Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu ndani ya Kristo Yesu yaliyoko Yudea. Mliteswa na watu wenu wenyewe kama vile makanisa hayo yalivyoteswa na Wayahudi. 15 Wao walimwua Bwana Yesu na manabii, wakatufukuza na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu na tena ni adui wa kila mtu kwa kuwa 16 wanajaribu kutuzuia tusiwahubirie watu wa mataifa mengine ujumbe ambao utawaokoa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia.

Paulo Atamani Kuwaona Wathesalonike

17 Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa muda, ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu si kwa moyo, tulizidi kwa hamu kubwa kufanya kila jitihada tuonane uso kwa uso. 18 Maana tulitaka kuja huko, hasa mimi Paulo, nilijaribu zaidi ya mara moja, lakini shetani akatuzuia. 19 Kwa maana ni nini tumaini letu, furaha yetu au taji yetu ya utukufu mbele za Bwana Yesu Kristo atakapokuja? Si ninyi? 20 Hakika ninyi ndio utukufu wetu na furaha yetu.