Haki Za Mtume

Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana. Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu. Je? hatuna haki ya kupewa chakula na cha kunywa? Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa? Au ni Barnaba na mimi tu ambao tunal azimika kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?

Ni askari yupi anayelipa gharama zake mwenyewe akiwa kam bini? Ni mkulima gani anayepanda mizabibu na hali matunda yake? Ni mfugaji yupi asiyekunywa maziwa ya kundi la wanyama wake? Mnadhani nasema haya kwa kutumia mifano ya kila siku tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? Kwa maana sheria ya Musa inasema, “Usimfunge ng’ombe kinywa wakati anapopura nafaka.” Je? Mnad hani ni ng’ombe ambaye Mungu anamfikiria? 10 Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Kwa kweli haya yalisemwa kwa ajili yetu kwa sababu mtu anapolima na mwingine akapura nafaka, wote wana paswa kufanya hivyo wakiwa na matumaini ya kupata sehemu ya mavuno. 11 Je, ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, itakuwa ni kitu kikubwa sana iwapo tutavuna mahitaji ya mwili kutoka kwenu? 12 Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, sisi je, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi? Lakini sisi hatukupenda kutumia haki hii, bali tunavumilia kila kitu ili tusije tukaweka kizuizi kwenye Injili ya Kristo.

13 Hamjui kwamba, watu walioajiriwa kazi Hekaluni wanapata chak ula chao hekaluni, na wale wanaohudumu madhabahuni wanapata sehemu ya sadaka zinazotolewa? 14 Vivyo hivyo, Bwana aliagiza kwamba wale wanaohubiri Injili watapata chakula chao kutokana na Injili. 15 Lakini mimi sikutumia haki hizi, na wala siandiki haya ili kudai haki zangu. Ni afadhali nife, kuliko mtu aniondolee haki hii ya kujisifu. 16 Ninapohubiri Injili, siwezi kujisifu kwa sababu ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipohubiri Injili! 17 Nikihubiri kwa hiari ningetegemea kupata tuzo; lakini ikiwa nalazimika kufanya hivyo, basi ninachofanya ni kutekeleza wajibu wangu. 18 Kwa hali hii tuzo yangu ni nini? Tuzo yangu ni hii, kwamba katika kuhubiri kwangu, nitangaze Injili pasipo kudai cho chote na hivyo nisitumie haki zangu katika kuhubiri Injili.

19 Ingawa mimi ni huru, na si mtumwa wa mtu ye yote, nimeji fanya kuwa mtumwa wa wote, ili niweze kuwavuta wengi iwezeka navyo. 20 Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi ili niweze kuwa vuta Wayahudi. Kwa watu wanaotawaliwa na sheria, nilikuwa kama niliye chini ya sheria, ingawa mimi siko chini ya sheria, ili niweze kuwavuta walio chini ya sheria. 21 Kwa watu wasioijua sheria nilikuwa kama nisiye na sheria, ingawa hii haina maana kwamba sizishiki amri za Mungu, bali niko chini ya sheria ya Kristo, ili niweze kuwavuta wasio na sheria. 22 Kwa wadhaifu nilikuwa mdhaifu ili niweze kuwavuta wadhaifu. Nimekuwa mdhaifu ili niweze kuwavuta wadhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi yao. 23 Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nishiriki baraka zake.

24 Mnajua kwamba katika mashindano ya riadha wote wanao shindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu anayepata tuzo. Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa njia itakayowapatia tuzo. 25 Kila mwana-riadha anayeshiriki katika michezo ya mashindano hufanya mazoezi makali. Wanafanya hivyo ili kupokea tuzo ambayo haidumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata tuzo isiyohari bika kamwe. 26 Mimi sikimbii pasipo kuwa na lengo. Sipigani kama mtu anayepiga hewa; 27 lakini nauimarisha mwili wangu na kuutawala, ili baada ya kuwahubiria wengine, mimi mwenyewe nisije nikakataliwa.