1 Wakorintho 8-10
Neno: Bibilia Takatifu
Chakula Kilichotolewa Sadaka Kwa Sanamu
8 Sasa kuhusu chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Tuna jua kwamba ‘sisi sote tuna ujuzi.’ Lakini ‘ujuzi’ huleta maji vuno, ila upendo hujenga. 2 Mtu anayedhania kwamba anajua kitu, basi hajafahamu kama inavyompasa kujua. 3 Lakini kama mtu anam penda Mungu, mtu huyo anajulikana na Mungu.
4 Kwa hiyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua kwamba ‘sanamu haina uhai wa kweli’ na kwamba ‘kuna Mungu mmoja tu.’ 5 Kwa maana hata kama wapo hao wanaoitwa ‘miungu,’ kama ni mbinguni au duniani; na kwa kweli wapo ‘miungu’ wengi na ‘mabwana’ wengi; 6 sisi tunajua kwamba kuna Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vinatoka kwake, na sisi tunaishi kwa ajili yake; na kuna Bwana mmoja, Yesu Kristo, ambaye vitu vyote vimekuwepo kupitia kwake na tunaishi kutokana naye.
7 Lakini si wote wanajua mambo haya. Watu wengine mpaka leo bado wamezoea miungu ya sanamu kiasi ambacho wanapokula chakula hicho wanadhani ni chakula kilichotolewa kwa sanamu, na kwa kuwa dhamiri yao ni dhaifu, inadhurika. 8 Lakini chakula hakitusaidii kuwa karibu zaidi na Mungu. Hatupotezi cho chote tusipokula, wala hatupati faida yo yote kama tukila.
9 Lakini hata hivyo tuwe waangalifu jinsi tunavyotumia uhuru wetu tusije tukawakwaza walio dhaifu katika imani. 10 Kwa maana kama mtu mwenye dhamiri dhaifu akiwaona ninyi wenye ujuzi mkila katika hekalu la sanamu, je, si atavutwa kula chakula kilichoto lewa kwa sanamu? 11 Kwa njia hiyo, huyo ndugu mwenye dhamiri dhaifu, ambaye Kristo alimfia, atateketea kwa sababu ya ujuzi wako. 12 Mnapowatenda dhambi ndugu zenu kwa njia hii na kuharibu dhamiri zao dhaifu, mnamkosea Kristo. 13 Kwa hiyo kama chakula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke.
Haki Za Mtume
9 Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? 2 Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana. 3 Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu. 4 Je? hatuna haki ya kupewa chakula na cha kunywa? 5 Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa? 6 Au ni Barnaba na mimi tu ambao tunal azimika kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?
7 Ni askari yupi anayelipa gharama zake mwenyewe akiwa kam bini? Ni mkulima gani anayepanda mizabibu na hali matunda yake? Ni mfugaji yupi asiyekunywa maziwa ya kundi la wanyama wake? 8 Mnadhani nasema haya kwa kutumia mifano ya kila siku tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? 9 Kwa maana sheria ya Musa inasema, “Usimfunge ng’ombe kinywa wakati anapopura nafaka.” Je? Mnad hani ni ng’ombe ambaye Mungu anamfikiria? 10 Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Kwa kweli haya yalisemwa kwa ajili yetu kwa sababu mtu anapolima na mwingine akapura nafaka, wote wana paswa kufanya hivyo wakiwa na matumaini ya kupata sehemu ya mavuno. 11 Je, ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, itakuwa ni kitu kikubwa sana iwapo tutavuna mahitaji ya mwili kutoka kwenu? 12 Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, sisi je, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi? Lakini sisi hatukupenda kutumia haki hii, bali tunavumilia kila kitu ili tusije tukaweka kizuizi kwenye Injili ya Kristo.
13 Hamjui kwamba, watu walioajiriwa kazi Hekaluni wanapata chak ula chao hekaluni, na wale wanaohudumu madhabahuni wanapata sehemu ya sadaka zinazotolewa? 14 Vivyo hivyo, Bwana aliagiza kwamba wale wanaohubiri Injili watapata chakula chao kutokana na Injili. 15 Lakini mimi sikutumia haki hizi, na wala siandiki haya ili kudai haki zangu. Ni afadhali nife, kuliko mtu aniondolee haki hii ya kujisifu. 16 Ninapohubiri Injili, siwezi kujisifu kwa sababu ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipohubiri Injili! 17 Nikihubiri kwa hiari ningetegemea kupata tuzo; lakini ikiwa nalazimika kufanya hivyo, basi ninachofanya ni kutekeleza wajibu wangu. 18 Kwa hali hii tuzo yangu ni nini? Tuzo yangu ni hii, kwamba katika kuhubiri kwangu, nitangaze Injili pasipo kudai cho chote na hivyo nisitumie haki zangu katika kuhubiri Injili.
19 Ingawa mimi ni huru, na si mtumwa wa mtu ye yote, nimeji fanya kuwa mtumwa wa wote, ili niweze kuwavuta wengi iwezeka navyo. 20 Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi ili niweze kuwa vuta Wayahudi. Kwa watu wanaotawaliwa na sheria, nilikuwa kama niliye chini ya sheria, ingawa mimi siko chini ya sheria, ili niweze kuwavuta walio chini ya sheria. 21 Kwa watu wasioijua sheria nilikuwa kama nisiye na sheria, ingawa hii haina maana kwamba sizishiki amri za Mungu, bali niko chini ya sheria ya Kristo, ili niweze kuwavuta wasio na sheria. 22 Kwa wadhaifu nilikuwa mdhaifu ili niweze kuwavuta wadhaifu. Nimekuwa mdhaifu ili niweze kuwavuta wadhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi yao. 23 Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nishiriki baraka zake.
24 Mnajua kwamba katika mashindano ya riadha wote wanao shindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu anayepata tuzo. Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa njia itakayowapatia tuzo. 25 Kila mwana-riadha anayeshiriki katika michezo ya mashindano hufanya mazoezi makali. Wanafanya hivyo ili kupokea tuzo ambayo haidumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata tuzo isiyohari bika kamwe. 26 Mimi sikimbii pasipo kuwa na lengo. Sipigani kama mtu anayepiga hewa; 27 lakini nauimarisha mwili wangu na kuutawala, ili baada ya kuwahubiria wengine, mimi mwenyewe nisije nikakataliwa.
Mafundisho Kutoka Historia Ya Wayahudi
10 Nataka mkumbuke ndugu zangu, kwamba baba zetu wote wali kuwa wakiongozwa na wingu, na wote walipita katikati ya bahari ya Shamu. 2 Wote walibatizwa kama wafuasi wa Musa katika lile wingu na ndani ya ile bahari. 3 Wote walikula kile chakula cha kiroho, 4 na wote walikunywa kile kinywaji cha kiroho. Kwa maana waliku nywa kutoka katika ule mwamba wa kiroho uliofuatana nao; na mwamba huo ulikuwa ni Kristo. 5 Hata hivyo Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo maiti zao zilitapakaa jangwani.
6 Basi mambo haya ni onyo kwetu, tusitamani uovu kama wao walivyofanya. 7 Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyofa nya. Kama Maandiko yasemavyo, “Watu walikaa chini wakala na kunywa, kisha wakainuka kucheza.” 8 Wala tusifanye uasherati kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. 9 Pia tusimjaribu Bwana, kama wengine walivyofa nya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 Msilalamike, kama wengine walivyofanya, wakaangamizwa na malaika wa kifo.
11 Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wen gine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.
12 Kwa hiyo mtu anayejidhania kwamba anasimama, awe na tahadhari asije akaanguka. 13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.
14 Kwa hiyo rafiki zangu, msishiriki katika ibada za sanamu. 15 Nasema nanyi kama na watu wenye ufahamu. Amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 16 Je? Kikombe cha baraka ambacho tuna kibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Na mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa kuna mkate mmoja, sisi tulio wengi, tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki mkate mmoja. 18 Fikirini kuhusu Waisraeli, je, Wanaokula kilichotolewa sadaka hawashiriki katika madhabahu? 19 Je, nikisema hivyo nina taka kusema kwamba sadaka iliyotolewa kwa sanamu au kwamba sanamu ina maana yo yote? 20 La, sivyo. Lakini sadaka inayotolewa kwa sanamu inatolewa kwa mashetani, na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muwe na ushirika na mashetani. 21 Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na kunywa katika kikombe cha mashetani pia. Hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya mashe tani. 22 Je, tunataka kujaribu kumfanya Bwana awe na wivu? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?
Uhuru Wa Mwamini
23 Vitu vyote vinaruhusiwa, lakini si vitu vyote vina faida. ‘Vitu vyote ni halali,’ lakini si vyote vinajenga. 24 Mtu asita fute yale yanayomfaa yeye peke yake, bali atafute yale yanayomfaa jirani yake.
25 Kuleni cho chote kinachouzwa katika masoko ya nyama bila kuuliza maswali kuhusu dhamiri. 26 Kwa maana, ‘Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.’ 27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kitakachokuwa mezani bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama ukiam biwa, “Hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu,” basi kwa ajili ya huyo aliyekuambia juu ya hicho chakula, na kwa ajili ya dhamiri, usile. 29 Namaanisha dhamiri ya huyo aliyekuambia, si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30 Kama nakula kwa shukrani, kwa nini nashutu miwa kwa kile ambacho ninatoa shukrani?
31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kik wazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki, au kwa kanisa la Mungu; 33 kama mimi ninavyojaribu kumridhisha kila mtu katika kila kitu ninachofanya. Kwa maana sitafuti kujiridhisha mwenyewe bali nata futa faida ya walio wengi, ili waweze kuokolewa.
Copyright © 1989 by Biblica