Add parallel Print Page Options

Sikumbuki kosa lolote nililofanya, lakini hiyo hainifanyi mimi kujihesabia haki. Bwana pekee ndiye anayepaswa kunihukumu ikiwa nimefanya vyema au la. Hivyo, msimhukumu mtu yeyote sasa. Hukumu itakuwa wakati Bwana atakaporudi. Ataangaza mwanga kwa kila kitu kilichofichwa gizani. Ataziweka wazi nia za siri za mioyo yetu. Ndipo sifa ambayo kila mtu anapaswa kuipata itatoka kwa Mungu.

Ndugu zangu, nimemtumia Apolo na mimi mwenyewe kama mfano kwa ajili yenu. Nimefanya hivi ili mjifunze kutoka kwetu maana ya maneno yanayosema, “Uwe mwangalifu kufuata kilichoandikwa.”[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 4:6 Uwe mwangalifu kufuata kilichoandikwa Kwa maana ya kawaida, “Msifanye zaidi ya kile kilichoandikwa”. Hii ina maana ya Maandiko ama usemi maarufu, mfumo ama kanuni kwamba walimu walitumia watoto kuandika alfabeti. Paulo anawatia moyo Wakorintho wafuate mfano huo.