Dhamiri yangu hainishitaki; lakini hilo halinifanyi nisiwe na hatia. Bwana ndiye anayenihukumu. Kwa hiyo msitoe hukumu kabla ya wakati wake, kabla Bwana hajaja. Yeye atafichua mambo yaliyof ichwa gizani na kwa kuweka wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mtu atapokea sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.

Basi ndugu zangu nimetumia mfano wa Apolo na mimi kwa faida yenu ili muweze kujifunza kutoka kwetu maana ya usemi, “Usivuke mpaka wa yale yaliyoandikwa.” Na hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine.

Read full chapter